Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa kampuni ya Simu ya Airtel, mazungumzo hayo yamefanyika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma Tarehe 10 Aprili,2019.
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Kampuni ya Simu za Mkononi Airtel nchini, wapili kutoka kushoto ni Mwanasheria wa Bharti Airtel Bw. Mukesh Bhavnani, wa kwanza kulia Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bw. Sunil Colaso na wakwanza kilia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) leo tarehe 10 Aprili,2019 Jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Simu za Mkononi Airtel ukiongozwa na Bw. Mukesh Bhavnani, Mwanasheria wa Bharti Airtel, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bw. Sunil Colaso na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano.
Katika mazungumzo hayo, Uongozi wa Airtel umemuhakikishia Mheshimiwa Kabudi kuwa Kampuni ya Bharti Airtel itaendelea kuwa Mbia mzuri na Serikali na kwamba wataendelea kupanua wigo wa huduma zao katika maeneo yote nchini na kuhakikisha hudua hizo zinakuwa za viwango na nafuu kwa watumiaji. Na kwamba mpango wao wa uwekezaji na kupanua wigo wa huduma zao hususan maeneo ya vijijini utakuwa moja ya chachu ya maendeleo ya kiuchumi nchini.
Kwa upande wake, Mheshimiwa Kabudi pamoja na kuwashukuru kwa kumtembelea ameihakikishia Bharti Airtel kuwa Serikali iko tayari kuendelea na ubia walionao na iko tayari kuendelea kushauriana na kushirikiana namna bora ya kuimarisha ubia huo ili kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa na viwango na zinafika katika maeneo mengi nchini kwa gharama nafuu.
No comments:
Post a Comment