Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Bw. Tito Haule, akifungua Kikao cha Wadau wa Vyama vya Ushirika nchini kujadili taarifa ya uhakiki wa takwimu za Vyama vya Ushirika.
Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Tathmini wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Buji Bampebuye, akitoa mada kwenye Kikao cha Wadau wa Vyama vya Ushirika nchini kujadili taarifa ya uhakiki wa takwimu za Vyama vya Ushirika.
Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Josephat Kisamalala, akitoa mada kwenye Kikao cha Wadau wa Vyama vya Ushirika nchini kujadili taarifa ya uhakiki wa takwimu za Vyama vya Ushirika
Wadau wa Ushirika wakiwa kwenye Kikao cha Wadau wa Vyama vya Ushirika nchini kujadili taarifa ya uhakiki wa takwimu za Vyama vya Ushirika.
Kikao cha Wadau wa Vyama vya Ushirika nchini kimefanyika leo Jumatatu, Aprili 15, 2019 Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili taarifa ya uhakiki wa takwimu za Vyama vya Ushirika na kutoa maazimio juu ya majukumu yanayopaswa kutekelezwa na kila mdau kulingana na matokeo na changamoto zilizobainishwa. Taarifa hii itasaidia katika kuboresha utendaji kazi wa Vyama vya Ushirika nchini.
Akifungua kikao hicho, Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Bw. Tito Haule amesisitiza umuhimu wa kuwa na takwimu sahihi za Vyama vya Ushirika na amewataka wadau wa ushirika nchini kutotoa takwimu za Vyama vya Ushirika bila kuwasiliana na mamlaka husika ambayo ni Tume ya Maendeleo ya Maendeleo ya Ushirika.
Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania ilifanya zoezi la uhakiki wa Takwimu za Vyama vya Ushirika nchini na kupanga SACCOS kwenye madaraja (SACCOS Categorization) mwaka 2018 ili kupata takwimu sahihi za Vyama vya Ushirika. Zoezi hilo lilikamilika mwishoni mwa mwaka 2018 na taarifa ya uhakiki huo iliandaliwa ambayo imesaidia kupata takwimu halisi za vyama hivyo.
No comments:
Post a Comment