Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza katika hafla ya kuwapongeza wahitimu wa mafunzo ya Stashahada ya Juu ya Masuala ya Uongozi inayotolewa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha AALTO cha nchini Finland, iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Prof. Joseph Semboja akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kuzungumza na wahitimu wa mafunzo ya Stashahada ya Juu ya Masuala ya Uongozi katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimpongeza mmoja wa watumishi kutoka Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Leonce Temba baada ya kuhitimu mafunzo ya Stashahada ya Juu ya Masuala ya Uongozi katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amewataka wahitimu wa mafunzo ya Stashahada ya Juu ya Masuala ya Uongozi kutumia vizuri ujuzi walioupata ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na hatimaye kuchangia katika maendeleo ya Taifa.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa (Mb) amesema hayo, alipokuwa akizungumza katika hafla ya kuwapongeza wahitimu wa Stashahada ya Juu ya Masuala ya Uongozi iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema anatarajia wahitimu hao kuwa mfano bora wa kuigwa katika jamii kwa kusimamia vema masuala ya utawala bora, haki za binadamu, utawala wa sheria huku wakionyesha uzalendo na ufanisi wa hali ya juu katika shughuli zao za kila siku.
“Nina imani kuwa mafunzo haya yamewabadilisha kifikra na kimtazamo katika masuala yote yanayohusu uongozi na mmekuwa na uelewa mpana utakaobadili utendaji kazi wenu kutokana na programu hii iliyofundishwa na wataalamu wabobezi wa hapa nchini na nje ya nchi,” Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameongeza kuwa, serikali inategemea kuona kwa vitendo kile walichojifunza darasani kwa kipindi cha mwaka mmoja ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa kuzingatia uzalendo na uadilifu mkubwa na kuwa na uongozi wa kimkakati kwa kusimamia vizuri rasilimaliwatu na rasilimali fedha.
Akizungumza kwa niaba ya wahitimu, Bi. Neema Mwakalyelye ameahidi kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Mhe. Dkt. Mwanjelwa na kusema kuwa watakuwa viongozi bora wanaopenda mabadiliko chanya ili kutimiza dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025.
Aidha, ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuruhusu watumishi kuhudhuria mafunzo hayo na Serikali ya Finland kwa kudhamini na hatimaye kufanikisha uwepo wa mafunzo hayo nchini Tanzania.
Jumla ya wahitimu 33 wakimemo baadhi ya viongozi wastaafu wa serikali na viongozi waandamizi serikalini walitunukiwa vyeti vya Stashada ya Juu ya Masuala ya Uongozi yanayotolewa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha AALTO cha nchini Finland.
IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
TAREHE 10 APRILI, 2019

No comments:
Post a Comment