Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akiongea na wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali ambao kwa pamoja wanaunda kikosi kazi cha kusimamia utekelezaji wa katazo la mifuko ya plastiki hapa nchini. Wajumbe hao ni kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mamlaka ya Mapato Tanzania, Idara ya Uhamiaji, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Shirika la Viwango Tanzania, Mamlaka ya Chakula na Dawa, Jeshi la Polisi, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Kikao hicho kimefanyika hii leo katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango – Dodoma.
Sehemu ya wajumbe wanaounda kikosi kazi cha kusimamia utekelezaji wa katazo la mifuko ya plastiki hapa nchini wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba (Hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika hii leo katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango.
No comments:
Post a Comment