Dodoma. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na naibu wake, Juliana Shonza kutoambatana na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri, maandalizi duni ya timu hiyo na kutotengewa fedha na Serikali ya Tanzania, ni mambo yaliyotikisa Bunge leo Jumanne Juni 25, 2019.
Wabunge wamehoji mambo hayo matatu baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu na Spika, Job Ndugai kulazimika kumpa nafasi Dk Mwakyembe kutoa majibu ambayo pia hayakuwaridhisha wawakilishi hao wa wananchi.
Wakati Dk Mwakyembe akisema Ndugai aliyekwenda Misri pamoja na wabunge 50 alimuwakilisha vyema, Spika huyo amesema Dk Mwakyembe na naibu wake kutokwenda Misri hakuleti picha nzuri, kutaka Serikali ya Tanzania katika bajeti yake ya 2020/2021 kutenga fedha kwa ajili ya timu hiyo.
Katika fainali hizo Taifa Stars ipo kundi moja na Senegal, Kenya na Algeria. Tayari imeshacheza mchezo wa kwanza na kufungwa mabao 2-0 na Senegal.
Huku akieleza safari ya wabunge wengine 30 watakaokwenda Misri kesho baada ya wengine 50 kurejea jana, Ndugai aliwataka wananchi wengine kwenda kuishangilia Taifa Stars na kusisitiza kuwa katika kambi ya timu hiyo Misri, kuna mambo hayapo vizuri.
“Tutaongea na waziri mkuu (Kassim Majaliwa) na Waziri wa Michezo katika bajeti zinazokuja ikiwezekana mwakani tutajipanga vizuri zaidi lazima waziri wa fedha atenge fedha kwa ajili ya timu ya Taifa,”
No comments:
Post a Comment