ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 2, 2019

CGF ANDENGENYE APOKEA MSAADA WA VIFAA VYA KUZIMIA MOTO NA MAOKOZI

 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye, akipokea Sare za kuzimia moto (Fire suite), kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Wilna International Japan, Bw. Martin Chuwa. Vifaa hivyo vimepokelewa Makao mapema hii leo Makuu Ndogo ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye, akipokea Mikanda maalum kwa ajili ya maokozi (Rescue Belt), kutoka Mwakilishi wa Kampuni ya Wilna International Japan, Bw. Martin Chuwa. Vifaa hivyo vimepokelewa mapema hii leo Makao Makuu Ndogo ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya vifaa vya kuzimia moto na maokozi vilivyotolewa na Kampuni ya Wilna International Japan na kukabidhiwa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa Lengo la kuboresha utendaji kazi. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, CGF Thobias Andengenye, amepokea msaada wa vifaa vya kuzimia moto na maokozi vitakavyotumika kwa shughuli mbalimbali za Jeshi hilo.

Amepokea msaada huo mapema hii leo Makao Makuu Ndogo ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam, kutoka kwa Kampuni ya Wilna International Japan.
Hata hivyo, Andengenye ameishukuru Kampuni hiyo kwa kutoa msaada huo na kushirikiana na Jeshi hilo katika Kuokoa Maisha na Mali za Watanzania.   
Aidha, Mwakilishi wa Kampuni ya Wilna International Japan, Bw. Martin Chuwa, amesema kuwa wameamua kutoa msaada huo wa vifaa vya kuzimia moto na maokozi ili kurahisisha utendaji kazi wa Jeshi hilo.

No comments: