Viongozi wa Shirika lisilo la Kiserikali la HEAD INC, wakutana na Naibu Waziri wa wizara ya mambo ya nje na ushiriano wa Kimataifa wa afrika ya mashariki, Mheshimiwa Dr. Damas Ndumbaro. Mheshimiwa Ndumbaro amewashukuru HEAD INC, kwa huduma za Afya wanazozitoa sehemu mbali mbali hapa nchini kila mwaka, takriban kwa miaka minne sasa.
Mwaka huu 2019 HEAD INC imetoa huduma na elimu ya afya kisiwani Pemba, katika hospitali ya Chake Chake na pia katika Hospitali Teule ya Muheza, mkoani Tanga.
Mhe Waziri amewataka watanzania, wana diaspora duniani waige mfano wa HEAD INC sambamba na mpango wa serikali ya awamu ya tano kufikisha huduma muhimu kwa kila Mtanzania.
No comments:
Post a Comment