Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (katikati), akiongoza Kikao cha Utendaji cha Maofisa Wakuu wa Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es salaam, kujadili utendaji wa kazi za Polisi, kufanya tathmini, Mafanikio, Changamoto na kuweka mikakati ya kutekeleza kazi za Polisi hususan kulinda maisha ya raia na mali zao, kushoto kwake ni Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii CP Mussa A. Mussa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas na kulia kwake ni Kamishna wa Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi CP Shabani Hiki na Kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu CP Benedict Wakulyamba.
Maofisa Wakuu wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi wakifuatilia hotuba inayotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCP Charles Kenyela (aliyesimama), Wakati wa Kikao cha Utendaji cha Maofisa Wakuu kilichofanyika jijini Dar es salaam na kujadili utendaji wa kazi za Polisi, kufanya tathmini, Mafanikio, Changamoto na kuweka mikakati ya kutekeleza kazi za Polisi hususan kulinda maisha ya raia na mali zao ili kuhakikisha jamii inakuwa salama. Picha na Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment