ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 30, 2019

JPM AFIKA KUTOA POLE KWA MBOWE ALIYEFIWA NA KAKA YAKE


Rais Magufuli akisaini kitabu cha rambirambi.

RAIS John Magufuli leo asubuhi amefika kutoa pole kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kufuatia kufiwa na kaka yake, Meja Jenerali Mbowe, Julai 28, 2019. Msiba upo nyumbani kwa marehemu Salasala jijini Dar es Salaam.
Magufuli akiwa miongoni mwa wafiwa.

Taarifa ya Ikulu ya leo Jumanne Julai 30, 2019, imesema Magufuli amekutana na kiongozi wa familia hiyo, Freeman Mbowe, ambako alishiriki sala ya kumuombea marehemu.
Mbowe (kulia) akimpokea Magufuli.

No comments: