ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 29, 2019

Ndayiragije: Tutajilaumu wenyewe

KOCHA wa timu ta Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mrundi Ettiene Ndayiragije 
By THOBISIAN SEBASTIAN, MWANASPOTI

KOCHA wa timu ta Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mrundi Ettiene Ndayiragije mara baada ya mechi na Harambee Stars, amesema walishindwa kutumia nafasi walizozitengeneza.

Ndayiragije aliyasema hayo baada ya mechi yao ya kwanza ya kuwania kufuzu fainali za Chan iliyochezwa jana Jumapili uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kutoka suluhu.

Alisema kikosi chake kilicheza vizuri kuanzia nyuma mpaka mbele kwa kutumia mbinu nyingi alizowaelekeza mazoezini lakini walishindwa kutumia nafasi za kufunga walizozitengeneza.
"Tulipata nafasi nyingi za kufunga vipindi vyote viwili ambazo kama tungekuwa na umakini mkubwa kama ule ambao tulikuwa tunautumia kutengeneza nafasi tungepata mabao,'

"Ukiangalia vipindi vyote viwili nafasi za kufunga tulitengeneza lakini tulionekana kuwa na umakini mdogo ambao ulisababisha tusifunge.

"Kwa muda tuliokuwa kambini kabla ya mchezo huu ilikuwa lazima kutokee makosa kama haya ambayo tunakwenda kuyafanyia kazi katika mazoezi yetu kabla ya mechi ya marudiano ambayo tutacheza ugenini," alisema Ndayiragije.

No comments: