ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 31, 2019

Katty Perry akutwa na hatia ya kunakili wimbo wa msanii mwingine

By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Los Angeles, Marekani. Ukishangaa ya wasanii wa Afrika kuigana nyimbo, jiandae kushangaa ya mwimbaji Katty Perry aliyekutwa na hatia ya kuiga wimbo wa ‘Joyful Noise’ ulioimbwa na mwimbaji wa Gospel Flame.

Perry amekutwa na hatia ya kutokuwa na hatimiliki ya ngoma ‘Dark Horse’ ambayo ilidaiwa kuwa iliigwa.

Kwa mujibu wa tovuti ya BBC kupitia ukurasa wa Newsround umeeleza kuwa Jumatatu Julai 29,2019 Mahakama mjini New York imethibitisha kuwa wimbo huo wa ‘Dark Horse’ uliotoka rasmi mwaka 2013 uliigwa kutoka kwenye wimbo wa ‘Joyful Noise’ ulioimbwa na mwimbaji anayetumia jina la Gospel Flame jukwaani huku jina lake halisi akiitwa Marcus Gray.

Pamoja na kukutwa na hatia hiyo mtayarishaji nyimbo wa Perry Dr Luke aliiambia mahakama kuwa hakuwahi kusikia wimbo wa ‘Joyful’ uliotoka mwaka 2009.

Katika utetezi wake, Perry alisema anaweza kuimba wimbo wake ‘Live’ mbele ya mahakama lakini ilishindikana kutokana na wakili wake kupata hitilafu ya vifaa na kushindwa kucheza ngoma ya ‘Dark Horse’.

BBC imeeleza mahakama imewatia hatiani watu sita akiwemo mwandaaji wa nyimbo mtunzi wa nyimbo Sarah Hudson na Juicy J na kuelezwa kuwa itawekwa wazi kiasi atakachotakiwa kulipa Katty Perry kwa Marcus Gray, kutokana na kunakili wimbo huo.

No comments: