GAVANA wa Kaunti ya Bomet, nchini Kenya, Joyce Laboso, amefariki leo Jumatatu Julai 29, 2019, wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Nairobi katika idara ya wagonjwa mahututi (ICU) kwa majuma mawil
Gavana huyo aliwahi kutibiwa London, Uingereza, kabla ya kuhamishiwa India kisha kurudishwa nyumbani Kenya na kupelekwa Nairobi Hospital ambako umauti umemkuta. Alikuwa miongoni mwa magavana watatu tu wa nchi hiyo, aliwahi kuwa Naibu Spika wa Bunge la Kenya.Hivi karibuni Julai 1, 2019, mbunge mwingine alifariki nchini Kenya kwa saratani ya damu. Kwa miaka ya hivi karibuni, Laboso amekuwa mtu maarufu wa tano kufariki kwa ugonjwa huo. Serikali ya nchi hiyo kupitia kwa mwanasiasa Raila Odinga imesema inajiandaa kujenga hospitali maalum kwa ajili ya kutibu na kushughulikia matatizo ya kansa nchini humo.
Laboso alizaliwa mwaka 1960. Mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Nairobi na serikali imesema itatangaza tarehe ya mazishi na taratibu za kuaga mwili huo.
Mumewe, Edwin Obonye, amesema anawaomba wananchi waipe familia muda wa kuomboleza huku akisema mkewe alibainika kuwa na ugonjwa huo miaka ya nyuma akatibiwa na akapata nafuu lakini hakutaka kuanika matatizo yake.
Laboso alikuwa Gavana aliyeamini katika ukombozi wa elimu na ndiyo maana aliwekeza zaidi katika elimu na bajeti yake ilijikita zaidi katika masuala ya elimu.
No comments:
Post a Comment