ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 3, 2019

Kigwangalla azuia magogo ya wafanyabiashara kwa miaka 2

Mkurugenzi wa Kirungi Kingalu Companya Limited, Kirungi Amir akionyesha nyaraka za Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Dar es Salaam hivi karibuni, wakati wa mahojiano na mwandishi gazeti hili. Picha na Elias Msuya

By Elias Msuya, Mwananchi emsuya@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kampuni ya Kirungi Kingalu inamlalamikia Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Khamis Kigwangalla kwa kuzuia shehena ya magogo ya mti aina mkurungu ambayo kampuni hiyo na kampuni nyingine zaidi ya 60 zilinunua kwenye mnada ulioendeshwa na Wakalwa Misitu Tanzania (TFS) mwaka 2017.

Waziri Kigwangalla alipoulizwa kwa simu, alisema kwamba amechukua uamuzi huo kwa kuwa miti hiyo ilivunwa kwa njia haramu.

“Tulizuia sababu ya taarifa za kiintelijensia zilizoeleza uwepo wa uvunaji haramu, hususan wa magogo ya mti wa mkurungu. Tukatuma kikosi kazi Taifa dhidi ya ujangili (NTAP), ambacho kimekamata magogo haramu yenye zaidi ya thamani ya Sh bilioni 10. Tumefanya uchambuzi wa kampuni zote zenye vibali na zilizo halali zimeruhusiwa. Bahati mbaya kampuni ya Kirungi Kingalu ina magogo yenye kesi, hivyo haikuruhusiwa,” alisema Dk Kigwangalla.

Mkurugenzi wa Kirungi Kingalu, Kirungi Amir amekiri sehemu ya shehena yake kukamatwa wilayani Kaliua mkoani Tabora na kufunguliwa kesi, lakini amehoji sababu ya Waziri Kigwangalla kuzuia sehemu kubwa ya shehena yake isiyo na kesi Bandari ya Tanga.

“Magogo yenye kesi yapo 385, hayo mengine anayazuilia nini? Mwizi akiwa na magari 10, kwenye msako unagundua mawili ya wizi unazuia na yale manane aliyonunua ki halali? Licha ya kwamba magogo yote yamelipiwa ikiwemo hayo anayosema yana kesi. Vinginevyo aseme zile risiti ni feki,” alisema Kirungi.

Mzozo ulipoanzia

No comments: