Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi akiongea kwenye mkutano wa jimbo akiwaeleza wapiga kura wake kwa namna gani amefanikiwa kutekeleza ilani ya CCM kama alivyoahidi wakati wa kumba kura kwa wananchi waliompa ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi Daudi Yassini akiwa na baadhi ya viongozi wa CCM wilaya ya Mufindi wakati wa upokea taarifa ya utelezaji ya Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi
Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi wilaya ya mufindi wakiwa makini kumsikiliza Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi wakati alipokuwa akiwasilisha mambo aliyoyafanya katika jimbo hilo kwa miaka mitatu aliyopo madarakani
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Wananchi wa jimbo la mafinga mjini
wamenufaika na matunda ya miaka mitatu madarakani ya mbunge Cosato Chumi kwa
ktekeleza ahadi zake kipindi cha uchaguzi wa mwaka 2015 kwa ujenzi wa Kituo cha
afya cha Ihongole, ujenzi wa Madarasa, mabweni na maabara katika shule za
Sekondari za Changarawe, Ihongole na JJ Mungai,kushughulikia swala la maji na
kufikisha umeme katika Vijiji vyote kumi na moja.
Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa
jimbo hilo Chumi alisema kuwa miradi ya Maendeleo katika Jimbo hilo ni pamoja
na ujenzi wa jengo la kisasa la Halmashauri ya Mji wa Mafinga ambalo liko
katika hatua za mwisho, ujenzi wa matanki ya maji katika Vijiji vya Maduma,
Bumilayinga, Kinyanambo na Changarawe ambako ujenzi wa tanki la ujazo wa
lita milioni moja unaendelea.
“Bado kuna changamoto katika baadhi
ya maeneo lakini yapo mengi yaliyofanyika ambayo ni wajibu wetu kuyasema tena
wazi wazi na kuwaelewesha wananchi kwa kuwa yanaonekana kwa macho na kuwaambia
kuwa changamoto zitatuliwa kulingana na muda wake hawezi kutatua changamoto
zote kwa pamoja” alisema Chumi
Chumi alisema kuwa alipokuwa anaingia
madarakani Mafinga hatukuwa na gari la uhakika la kubebea wagonjwa lakini kwa
kipindi cha miaka mitatu ya utawala wake amefanikisha upatikanaji wa magari
matatu ya kubebea wagonjwa (ambulance), vitanda na ultrasounds machine ambayo
inasaidia katika kuchunguza magonjwa ya kina mama Wajawazito
“wajibu wa kila mwanachama wa CCM
kueleza utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa wananchi wote mwananchi wa jimbo la mafinga atambue kazi
kubwa inayofanywa jimboni hapo au kwenye majimbo mengine” alisema Chumi
Aidha Chumi alisema kuwa kuna watu
ambao kazi yao ni kubeza na kuwapotosha wananchi kazi zinazofanywa na serikali
ya CCM,Sasa waelezeni wananchi kuwa ili kuongeza mapato ambayo yatatusaidia
kujenga barabara zetu, umeme kufika kila Kitongoji ndio maana Rais Magufuli
akaamua kununua ndege ili watalii wengi watembelee mbuga zetu na sisi tupate
fedha
“kukaa kimya na kutoeleza na kutafsri
faida kubwa ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya tano,nawaambia
ndugu zangu kazi kubwa inafanyika lakini bila sisi wana-CCM kueleza umma wa
watanzania, basi ni Sawa na bule au kutupa jiwe gizani bila kujua litamkuta
nani” alisema Chumi
Chumi amesema kuwa wapo wanaobeza kwa
kuwaambia wananchi kuwa miradi ya ujenzi wa Reli na ununuzi wa ndege haina
tija wakati miradi hiyo inaenda kuchochea ukuaji wa biashara na sekta
binafsi kwa ujumla.
“Anakuja mtu anakuambia Wewe treni ya
umeme utapanda lini, na Wewe mwana CCM unakaa kimya, hiyo sio Sawa, mueleze
wazi wazi kuwa ili tupate fedha, tunajenga reli ya kisasa ambayo itatumika
kusafirisha mizigo kwenda nchi za jirani ambazo hazina Bandari, na sisi
tutapata fedha ambazo zitagharamia elimu ya watoto wetu, tutajenga barabara za
lami, Tutafikisha umeme kila kona ya Mafinga na nchi yote, tutapata maji ya
uhakika” alisema
Kwa upande wake mwenyekiti wa
CCM wilaya ya Mufindi Daudi Yasini alimpongeza mbunge huyo kwa kazi aliyoifanya
ambayo inaonekana tofauti na kuwa na mbunge wa maneno maneno bila kazi kunekana.
No comments:
Post a Comment