RAIS wa Tunisia Beji Caid Essebsi amefariki alfajiri leo Julai 25, 2019 akiwa na umri wa miaka 92.
Essebsi ambaye alikuwa Rais wa kwanza wa nchi hiyo kuchaguliwa kidemokrasia, amefariki wakati akipatiwa matibabu kwenye hospitali ya kijeshi nchini humo.
Taarifa iliyotolewa na kijana wa Rais huyo Hafedh Caid imeeleza kuwa baba yake alikuwa kipatiwa matibabumara kwa mara tangu mwezi Juni mwaka huu wa 2019.
Kabla ya kushika nafasi hiyo Essebsi aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo waziri mkuu mwaka 2011 na baadaye kuwa Rais wa nchi hiyo.Pia amewahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2015 na hakutangaza nia ya kugombea nafasi ya kiti hicho katika uchaguzi utakaofanyika Novemba mwaka huu.
No comments:
Post a Comment