Mkurugenzi Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Mwajuma Magwiza akiongea wakati wa kufungua Mafunzo ya kujenga uwezo kwa wajane yaliyofanyika leo Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Mboni Mgaza akielezea malengo ya mafunzo wakati wa Mafunzo ya kujenga uwezo kwa wajane yaliyofanyika leo Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Idara ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Julius Mbilinyi akioelezea umuhimu wa kumuwezesha mjane kiuchumi wakati wa Mafunzo ya kujenga uwezo kwa wajane mafunzo yaliyofanyika leo Jijini Dodoma.
Mratibu wa Chama cha Wajane Tanzania (TAWIA) Kanda ya Mashariki Mariamu Aswile akitoa shukrani kwa niaba ya wajane wakati wa kufungua Mafunzo ya kujenga uwezo kwa wajane yaliyofanyika leo Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajane wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi
na maafisa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto mara baada ya ufunguzi wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo leo
Jijini Dodoma.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Serikali imewataka wajane kote Nchini kukumbuka kuhusu suala la
VVU/UKIMWI na kuwataka kuchukua tahadhari kupunguza maambukizi mapya
ya virusi vya UKIMWI kwa kutumia kinga, kuepuka tabia hatarishi,
kutokomeza unyanyapaa na ubaguzi kwa watu wanaoishi na virusi vya
UKIMWI.
Akiongea wakati wa kufungua Mafunzo ya kujenga uwezo kwa wajane
Mkurugenzi Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo
ya Jamii Mwajuma Magwiza alisema kuwa UKIMWI hadi sasa bado ni
janga la Kitaifa hivyo kusisitiza wajane hao kuchukua tahadhari kubwa
ili kuepukana maambukizi.
Aidha Magwiza pamoja na kuzungumzia maambukizi ya UKIMWI lakini
pia amesema tayari serikali kwa kushirikiana na wadau inaendelea
kuhamasisha jamii kuacha Mila na Desturi potofu za kunyanganya mali za
wajane, kuozesha watoto wakike katika umri mdogo ikiwemo kutakasa na
kurithi wajane.
Bi. Magwiza ameitaka jamii pia kuachana na mila zenye madhara kwa
mwanamke hususan mjane na zinazodhoofisha jitihada zake za kujikwamua
kifikra, kiutamaduni, kiuchumi na kijamii akiongeza kuwa kila mmoja
anao wajibu wa kutoa fursa sawa kwa makundi yote katika jamii ikiwemo
wajane kubadili fikra, mtizamo, kuwa jasiri, kujiamini na kutambua
kuwa mabadiliko yanaanza na wao.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu
Maendeleo ya Jamii Bi. Mboni Mugaza amewambia wajumbe wa Mafunzo hayo
kuwa lengo la Wizara yake ni kuwakutanisha wadau na viongozi wadini
ili waweze kujua huduma zinazotolewa na wajane lakini pia kuwajengea
uwezo ili waweze kukabiliana na changamoto za kimaisha ukizingatia
kuwa wengi wao ni wakuu wa familia.
Bi. Mariamu Aswile ambaye pia ni Mratibu wa Umoja wa Wajane Kanda ya
Mashariki akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na mafunzo hayo
amesema wosia ni jambo la Msingi kwa kulinda haki za wajane lakini pia
akasisitiza suala la mjane kupewa hati ya kifo ili iwe hatua muhimu ya
mjane husika kufuatilia mirathi itakayomsaidia kusaidia wazee.
Aidha Bi. Aswile amewata wananchi kufuatilia zaidi madhira na madhara
wayapatayo wajane ili na wao wasije yakawakuta matatizo ambayo
yanawakabili wajane kwa sasa kwani kila mmoja ni mjane mtarajiwa hivyo
ni muhimu kwa wajane watarajiwa na wapya kuhakikisha wanachukua
tahadhari kuepukena na madhara na changamoto za wajane walizonazo
sasa.
Wakati huohuo Mjane Bi. Stella Maveka kutoka kikundi cha Wajane
Tuinuane kilichopo mjini Dodoma ameyataja mafunzo hayo kuwa ya muhimu
kwa wajane kwani yatawasaidia wajane kujua taratibu za usajili wa
vikundi na wakati huo akilaani baadhi ya vyombo vya dora vinavyokamata
biashara za wajane na kuitaka serikali kuchukua hatua ili kuokoa
bidhaa hizo ambazo zinazuiliwa na mamlaka za serikali.
Mafunzo haya yanafanyika kufuatia agizo la Naibu Waziri Afya Dkt.
Faustine Ndugululile alilolitoa katika Kongamano la Wajane mapema
mwezi Juni Mwaka huu kwa Wizara yake kutaka Wajane wapatiwe mafunzo ya
ujasiliamali na vifungashio lakini pia namna bora ya kumiliki ardhi na
kwa wajane kupatiwa huduma ya Afya.
Utafiti uanaonesha kuwa kati ya 7% hadi 16% ya wanawake wote duniani
bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kupoteza haki ya
kumiliki mali , umasikini , mila na desturi za kuridhiwa baada
yakufiwa uku idadi ya wajane Tanzania ambao ni wa wanachama wa
TAWIA(Tanzania Widows Association) ikifikia 800,000.
No comments:
Post a Comment