Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Lugha Bashungwa amekutana na kufanya mazungumzo na Wadau mbalimbali kutoka Sekta binafsi na Serikali ikiwa ni muendelezo wa maandalizi ya Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe.
Katika kikao hicho wadau waliahidi kutoa ushirikiano unaohitajika ili kufanikisha maandalizi ya montano huo.
Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam tarehe 24 Julai, 2019.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akieleza hatua ziizofikiwa katika maandalizi ya Mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajiwa kufanyika nchini mwezi Agosti 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bwana Laurean Bwanakunu akichangia jambo katika kikao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye akizungumza
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe wakiwasikiliza wadau walipokuwa wakizungumza kwenye kikao hicho.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Agness Kayola (wa kwanza kushoto), Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Sheria wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Caroline Chipeta wakiwa kwenye mkutano uliowakutanisha Sekta Binafsi na Serikali
Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SportPesa, Bw. Abbas Tarimba naye akichangia mada katika kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bw. Albert Jonkergouw naye akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Juu na chini sehemu ya wadau kutoka Sekta Binafsi wakichangia mada kwenye Mkutano huo.
Dkt. Mnyepe akiendelea kuzungumza kwenye Mkutano huo.
No comments:
Post a Comment