Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mhe. Edward Mpogolo akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi wa utetezi dhidi ya mila potovu na udhalilishaji wa kijinsia uliofanyika wilayani humo mkoani Singida juzi. Mradi huo unasimamiwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Save Children for Central Tanzania (SMZZT). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Evalyen Lyimo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Save Mother and Children for Central Tanzania (SMZZT)Evalyen Lyimo akitoa taarifa ya utendaji katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa utetezi dhidi ya mila potovu na udhalilishaji wa kijinsia uliofanyika wilayani Ikungi mkoaniSingida juzi. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo, Haika Massawe na Mkuu wa Wilaya hiyo, Edward Mpogolo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mhe. Edward Mpogolo amewata viongozi wa madhehebu ya dini na mangariba wastaafu kushiriki kikamilifu vita dhidi ya vitendo vya ukeketaji Wilayani kwake.
Mhe. Mpogolo ameyasema hayo wakati akizindua mradi wa utetezi dhidi ya mila potofu ya ukeketaji na udhalilishaji uliofanyika hivi karibuni wilayani Ikungi mkoani humo.
Alisema utekelezaji sahihi wa masuala ya mila kwa mambo ya maendeleo ni jambo jema lakini inapokuwa kinyume kama masuala hayo ya ukeketaji inakuwa ni changamoto kubwa kwa jamii pia ni kinyume na haki za binadamu na Serikali kamwe haiwezi kuvumilia.
"Tuna taarifa kuwa ukeketaji wa sasa wanafanyiwa watoto wadogo na wachanga ambao hawawezi kukataa au kujihami na vitendo hivyo serikali haitaweza kuvumilia kuona vikiendelea na mtu yeyote atakaye baanika anavifanya atachukuliwa hatua kali" alisema Mpogolo.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Save the Mother and Children of Central Tanzania (SMCCT), Evalyene Lyimo alisema jumla ya wanawake na watoto 7, 648 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida wamekeketwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2016 na 2018.
"Kuanzia Januari hadi mwezi Oktoba 2018 jumla ya wanafunzi 37 wa Shule ya Sekondari wilayani humo walibainika kuwa na mimba huku wanawake na watoto 7,648 wakiwa wamekeketwa katika kipindi cha mwaka 2016 hadi 2018" alisema Lyimo.
Akizungumzia mradi huo Lyimo alisema ulianza mwaka 2017 hadi mwaka jana na kuwa katika kipindi hicho umetoa elimu juu ya madhara yatokanayo na mila potofu na udhalilishaji wa kijinsia kwa wakazi wapatao 15,000
No comments:
Post a Comment