ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 20, 2019

FURSA YA MAFUNZO KAZINI WILAYA YA IRINGA YAKUTANISHA ZAIDI YA WASOMI 514

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea na wasomi waliojitokeza ofisini kwake kwa ajili ya kuchangamkia fursa ya mafunzo kanzini inayotewa na serikari ya awamu ya tano
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela  akiwa katika akiwa amezungukwa na wasomi walijioteza kuchangamkia fursa ya mafunzo kazini 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela  akiwa katika akiwa amezungukwa na wasomi walijioteza kuchangamkia fursa ya mafunzo kazini 

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Zaidi ya wasomi mia tano na kumi na nne (514) wamejitokeza katika ofisi za mkuu wa wilaya ya Iringa kuchangamkia fursa iliyotolewa na serikali ya kuwasaidia wasomi kupata mafunzo kazini kwa mwaka mmoja na serikali itagharamia mafunzo hayo kwa kutoa kiasi cha shilingi laki moja na nusu kila mwenzi.

Akizungumza na blog hii Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano inayongozwa na Rais Dr John Pombe Magufuli imetenga fedha za kuwasaidia wasomi zaidi ya elfu tano nchi nzima kufanya kazi kwenye taasisi binafsi

“Mheshimiwa Rais ametanga fedha kupitia mfuko wa waziri mkuu kwa ajili ya kuwasaidia wasomi kufanya kazi kwenye mashirika binafsi kwa lengo la kuwasaidia kupata uzoefu kazini ili wakifanya vizuri waweze kusaidiwa na wengine kupata uzoefu ili wakienda kuomba kazi sehemu nyingine wawe na uzoefu” alisema Kasesela

Kasesela alisema kuwa alichokifanya ni kutimiza  ndoto ya Rais Dr John Pombe Magufuli ya kuhakikisha wasomi wote wanakuwa na uzoefu kazini kwa kuwawezesha ili kuwarahisisha kupata ajira pale wanapoenda kuomba kazi kwa kuwa watakuwa tayari wameshafanya kazi kwenye taasisi binafsi kwa mwaka mmoja.

“Ukiangalia Tanzania kada moja tu ya udaktari ndio kata ambayo imekuwa ikipewa mafunzo ya uzoefu kazini hivyo kada nyingine zote hazina mafunzo kazini ndio maana sisi wasaidizi wake tumeanza kutekeleza hili swala kwa nguvu zote” alisema Kasesela

Kasesela alisema kuwa aliitisha zoezi hilo huku akitegemea kuwa angepata wasomi wapatao mia moja tu lakini amekutana na wasomi mia tano na kumi na nne jambo ambalo hakulitarajia kukutana nalo.

“Nimekutana na wasomi wengi sana leo ambao wamesoma vitu tofauti tofauti na wanauwezo wa kufanya kazi hivyo ni jukumu langu kuwatafutia sehemu za kupata mafunzo kazini katika makampuni na mashirika yaliyopo wilaya ya Iringa”alisema Kasesela

Nao baadhi ya wasomi waliofika kwenye zoezi hilo wameipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr John Pombe Magufuli ikiwakilishwa vizuri na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa kuanzisha zoezi hilo.

“Kwa zoezi hili limetusaidia kwa kiasi kikubwa kupata uzoefu na kutusaidia kupata elimu ya mafunzo kazini na kusaidia njia rahisi ya kupata ajira kwa kuwa wasomi wanavyoenda kuomba kazi sehemu mbalimbali” alisema Kasesela

Wasomi hao walimpongeza Rais Dr John Pombe Magufuli kwa hatua aliyoichukua kuwatafutia njia mbadala ya kupata ajili kwa wasomi wengi ambao wapo mtaani hawana ajira. 

No comments: