Kampuni ya TBL chini ya kampuni ya Kimataifa ya ABInBev,imekabidhi masada wa vipuri vya kukarabati magari ya kituo cha polisi cha Ilala akiwa ni mwendelezo wake wa kuunga mkono jitihada za Serikali za kukabiliana na changamoto mbalimbali mojawapo ikiwa ni kuimarisha usalama kupitia kuboresha usafiri katika Jeshi hilo.
Msaada huo ulikabidhiwa na Meneja wa Kiwanda cha TBL cha Ilala, Calvin Martin na ulipokelewa naMkuu wa Kituo cha Polisi Ilala jijini Dar es Salaam, ASP Nyararo Otuma,ambaye alishukuru kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa kusaidia taasisi za Serikali sambamba na kufanya nazo kazi kwa kariibu katika kufanikisha kampeni mbalimbali zenye kunufaisha jamii.
Meneja wa kiwanda cha Ilala,Calvin Martin, alisema kuwa TBL, itaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kusaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali kama ambavyo imetoa vipuri (Shock Absorber) kwa ajili ya kufanikisha kutengeneza magari ya kituo cha Polisi cha Ilala, kwa ajili ya kuboresha usafiri wa askari wakati wa kutekeleza majukumu yake ya ulinzi na huduma mbalimbali katika jamii.
Aliongeza kusema kwa muda mrefu kampuni ya TBL imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Jeshi la Polisi katika kufanikisha kampeni zake mbalimbali za kijamii hususani zinazohusu usalama barabarani,kupinga vitendo vya Ukatili wa kijinsia na kampeni ya kuhamasisha matumizi yenye vinywaji vyenye kilevi kistaarabu.
Meneja wa kiwanda cha TBL ilala jijini Dar es Salaam, Calvin Martin, akiwa na wafanyanyakazi wa kiwanda hicho wakikabidhi masada wa vipuri kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Ilala jijini Dar es Salaam, ASP Nyararo Otuma,kwa ajili ya kuboresha usafiri wa Jeshi hilo.
Meneja wa masuala Endelevu wa TBL,Irene Mutiganzi na Mkuu wa Kituo cha Polisi Ilala jijini Dar es Salaam, ASP Nyararo Otuma, wakisaini nyaraka za makabidhiano ya vipuri hivyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Ilala, wakishuhudia makabidhiano hayo katika hafla iliyofanyika katika kiwandani.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Ilala jijini Dar es Salaam, ASP Nyararo Otuma, akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa TBL Ilala jijini Dar es Salaam Wakati wa hafla hiyo
No comments:
Post a Comment