ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 21, 2019

MBATIA ATUMIA JUBILEI YA MIAKA 25 YA KAKA YAKE KUSHAURI JAMBO SADEC.

Askofu wa Jimbo la Katoliki la Same,Mhashamu Rogathe Kimario akiongoza ya misa takatifu ya Jubilei ya fedha ya miaka 25 ya Padri Thomas Salekio Kesyy iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Yohani Mtume ,Parokia ya Iwa-Kirua Vunjo mkoani Kilimanjaro.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo, James Mbatia alikuwa miongoni mwa waumini walioshiriki Ibada hiyo ,ambapo Padri Thomas Kessy ni kaka yake mkubwa .
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika Ibada ya Misa ya takatifu ya Jubilei ya fedha ya miaka 25 ya Padri Thomas Kessy .
Padri Thomas Kessy akizungumza wakati wa ibada hiyo.
Baadhi ya ndugu wa Padri Thomas Kessy wakishiriki ibada hiyo.
Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitoa hotuba yake wakati wa ibada ya Misa takatifu ya Jubilei ya fedha ya kaka yake Padri Thomas Kessy .
Askofu wa Jimbo la Katoliki la Same,Mhashamu Rogathe Kimario akimkabidhi Padri Thomas Kessy sululu na vitu vingine vilivyotolewa kanisani hapo kama kumuunga mkono.
Baada ya kumalizika kwa misa hiyo ,shughuli ilihamia nyumbani kwa familia hiyo eneo la Kirua Vunjo wilaya ya Moshi.
Padri Thomas Kessy akiwaongoza ndugu zake kufungua Champegne wakati wa hafala fupi ya pongezi kwa Padri Thomas Kessy kufikisha miaka 25 ya utume.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akiwawekea wageni waalikwa kinywaji cha Champegne wakati wa hafla hiyo
Padri Thams Kessy akikata ndafu katika hafla hiyo.
Padri Thomas Kessy akimlisha kipande cha ndafu Askofu wa Jimbo la Katoliki la Same,Mhashamu Rogathe Kimario.
Baadhi ya wageni wakiwa katika hafla hiyo.
Wageni wakicheza muziki na Padri Thomas Kessy katika hafla hiyo hiy iliyofanyika nyumbani kwa familia ya Mbatia.
Na Dixon Busagaga .

MWENYEKITI wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) ambaye pia ni Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amewapa neno wakuu wa nchi 16 zinazounda Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), katika mkutano ujao kufikiria kuja na ajenda ya pamoja ya sera moja ya elimu inayofanana.

Mbatia amesema kuwa kama itakuwapo dhamira ya pamoja ya kuwa na sera hiyo ya elimu kwa wanachama wa SADC, kunaweza kubadili sura ya Afrika na mageuzi makubwa yakaonekana kwa miaka 20 yakisadifu mfumo wa elimu wa nchi za Ulaya.

Mbatia ametoa kauli hiyo mara baada ya kumalizika kwa ibada ya misa takatifu ya Jubilee ya fedha ya miaka 25 ya Padri Thomas Salekio Kessy, iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Yohani Mtume, Parokia ya Iwa-Kirua Vunjo, mkoani Kilimanjaro.

Ibada hiyo iliongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Same, Mhashamu Rogathe Kimario, akisaidiwa na Msimamizi wa Jimbo Katoliki la Moshi na Wakili wa Askofu, Deogratius Matiika.

“Kwa mfano, majuzi nilisikia na kusoma baadhi ya maandiko kwamba watu wa Namibia wao wanasema mfano mwanafunzi anayetoka Tanzania na amemaliza kidato cha sita na akienda kwao, kupata Chuo Kikuu kule ni shida, kwa sababu Namibia wao mfumo wao ni mgumu, wao elimu zao wanamalizia kidato cha nne. Unajiuliza hivi silabasi zetu zimeundwa namna gani, nawashauri wakuu wa nchi wanachama ni vizuri tukawa na sera moja ya SADC katika masuala ya elimu,”alisema

Mwaka huu, Tanzania imekuwa mwenyeji wa mkutano wa 39 wa SADC ikiwa imepita miaka 16, tangu mkutano kama huo kufanyika kwa mara ya mwisho mwaka 2003 chini ya utawala wa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.

Kuhusu Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, kuweka mikakati ya kuziwezesha nchi wanachama kufikia malengo ya kuelekea kwenye ukuaji wa uchumi wa kati utakaokuwa maendeleo ya viwanda, Mbatia alisema:

“Mimi nina ushauri kwa SADC, pamoja na mambo ya viwanda na mambo mengine yote ambayo ni muhimu, wakuu wa nchi 16 wajitahidi sana kuhakikisha nguvu kazi ya SADC ambayo ni vijana, wanapata elimu ambayo ni ujuzi na wanaweza kuzalisha kwenye viwanda, wanaweza kuondoa masuala ya umasikini, njaa, watu wakawa na afya njema lakini penda tusipende ni lazima tuangalie je mifumo yetu ya elimu ikoje,”alieleza

Alisema malengo hayo yanatekelezeka, lakini sharti nchi wanachama wawe wamejiandaa vizuri na kwa utafiti alioufanya, bado kuna kazi kubwa mbele ya safari, na akashauri zaidi kuwa malengo hayo yasiwe ya maneno, yaende kwenye vitendo zaidi

No comments: