ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 21, 2019

Yoweri Museveni na Paul Kagame wasaini makubaliano kumaliza mgogoro baina ya Uganda na Rwanda

Haki miliki ya picha IKULU RWANDA

Marais Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda wamesaini makubaliano ya amani katika mji mkuu wa Angola, Luanda kumaliza uhasama uliopo kati ya mataifa hayo jirani.

Walifikia makubaliano hayo katika mkutano wa pili huko Luanda mbele ya marais wa Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo , Angola na rais wa Congo Brazaville waliokuwa wapatanishi katika mgogoro huo.

Joto la kisiasa limekuwepo tangu mwanzoni mwa mwaka huu na limeathiri maisha ya watu kijamii na kiuchumi katika mataifa hayo jirani.

Maafisa nchini Rwanda wameishutumu Uganda kwa kuwafunga na kuwatesa kinyume cha sheria raia wake nchini Uganda, wakati Uganda nayo inaishutumu Rwanda kutekeleza ujasusi katika ardhi yake.

"Tutashughulikia matatizo haya yote". rais Kagame amewaambia wandishi habari baada ya kusaini makubaliano hayo. BBC

No comments: