ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 16, 2019

MBUNGE MGIMWA AKERWA NA UBOVU WA BARABARA ZA KATA YA MAPANDA


Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa kitongoji cha Mtwivila kilichopo kijiji cha Mapanda kata ya Mapanda juu ya masikitiko yake juu ya ubovu wa barabara
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa kitongoji cha Mtwivila kilichopo kijiji cha Mapanda kata ya Mapanda juu ya masikitiko yake juu ya ubovu wa barabara
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa kijiji cha Chogo kata ya Mapanda juu ya masikitiko yake juu ya ubovu wa barabara
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa kijiji cha Ihimbo kata ya Mapanda juu ya masikitiko yake juu ya ubovu wa barabara


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.


Wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini wanakabiliwa na changamoto ya ubovu wa miundombinu ya barabara ambayo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo kutokana na wananchi kutofanya kazi kwa uhuru.


Akizungumza wakati wa ziara yake kwenye kata ya Mapanda Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa amekiwa kuwa tatizo la ubovu wa miundombinu hiyo imekuwa kero na ameanza kuifanyia kazi ili kuzikarabati ziweze kupitika kirahisi.


“Nimebaini kuwepo kwa uchakavu wa barabara katika kata ya Mapanda ambazo zimekuwa zikififisha maendeleo ya jimbo langu hivyo natakiwa kufanya kila niwezalo kuhakikisha barabara hizi zinapitika” alisema Mgimwa


Mgimwa amesema kuwa amefaikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutengeza barabara zote korofi ili ziweze kupitika kwa urahisi.


“Nimefakisha kupata zaidi ya shilingi milioni mia nane kuhakikisha tunakarabati barabara hii ambayo imekuwa inatumiwa na watu wengi kimaendeleo katika jimbo hili” alisema Mgimwa


Mgimwaalisema kuwa kuna barabara inayotoka kuanzia Kibengu,Kipanga,Ihimbo,Uhafiwa,Kisusa,Ukami hadi njia panda ya Mapanda inayokadiliwa kuwa na urefu wa kilometa sitini na moja imetengewa fedha kidogo tofauti na matengenezo yanayotakiwa kufanyika katika barabara hiyo.


“Nitakuja na viongozi wa TARURA huku kuhakikisha wanajionea ubo vu wa barabara hizi ili wanavyotenga fedha wajue wanakarabati wapi na wanaacha wapi haiwezekani barabara hii ikatengewa kiasi cha shilingi milioni thelethini tu” alisema Mgimwa


Aidha Mgimwa amewataka TANROAD na TARURA kuzikarabati barabara zote korofi kipindi cha kiangazi ili zipitike kirahisi na sio kipindi cha masika ambapo mara nyingi hutokea kero kwa wananchi.


Wakitoa kilio chao kwa mbunge huyo wanachi wa vijiji hivyo walimwambia hakuna maendeleo yanayoendelea katika vijiji hivyo kutokana na ubovu wa barabara hizo.


Hakuna usafiri wa basi wala gari inayofika huku kutokana na ubovu wa barabara hizi hivyo tunakuomba uhakikishe unatusaidia kuzikarabati barabara hizo” walisema wananchi 

No comments: