Diwani wa kata ya Kihesa Jully Sawani akiongea na mwandishi wa habari wa blog hii ofisini kwake
NA
FREDY MGUNDA,IRINGA.
Mbunge
wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati ametakiwa kutimiza ahadi ya
kukarabati shule ya msingi Kihesa kama alivyowaahidi wakazi wa kata ya kisheza
wakati wa mkutano wa hadhara uliyofanyika katika shule hiyo.
Akizungumza
na blog diwani wa kata ya Kihesa Jully Sawani amemuomba mbunge huyo kutimiza
ahadi aliyoitoa kwa lengo la kuhakikisha wanaboresha sekta ya elimu katika kata
hiyo.
“Naomba
nimpongeze bwana Jose Mgongolwa kwa kusaidia kukarabati baadhi ya majengo ya
madarasa kwa msaada wake wa kukarabati madarasa hayo katika shule ya msingi
Kihesa” alisema Sawani
Kwa upande
wake Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati amesema kuwa atatimiza
ahdi hiyo mwezi wa tisa akitoka bungeni na kila kitu kipo sawa.
“Utaratibu
wa sasa ukiomba pesa kwa wadau unatakiwa kutoa account ya Halmashuri ili kila
kitu kinapitia kwenye ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri hivyo tayari wadau
tayari wameshazitoa na zipo halmashuri” alisema Kabati
Aidha
Kabati amesema anamifuko ya saruji zaidi ya mia saba kwa lengo la kukamilisha
ahadi zote alizoahidi katika shule mbalimbali mkoani Iringa.
Mwezi
wa tisa naanza kutekeleza ahdi zote kwa kuwa pesa ninazo hivyo ni jukumi la
mkurugenzi kuninunulia mifuko hiyo ya sariji ili nianze kutimiza ahadi zote.
No comments:
Post a Comment