NYATI FC SUMMER 2019 BBQ
kwa msimu wa pili mambo yalikuwa moto. Kama ulikosa wala usijutie kwani siku azigandi msimu wa tatu mambo yatakuwa ya kiongezeka zaidi na zaidi. Pata Taswira ya kila kilichoendelea kwenye BBQ hiyo hapa chini kiro safi.
Pongezi kwa vote waliochangia na waliofanikiwa kufika na kufurahi pamoja na familia, kwani shughuri ni watu na watu wenyewe ndiyo wewe na mimi.
Mwenyekiti wa Tanzania New York Community Bwana Seif Akida alikuwa sambamba na vijana wa Nyati Fc kuanzia mwanzo hadi mwisho shukrani mwenyekiti kwa support yako kwa vijana wa Nyati Fc.
Hansi na Richard wakipata ukodak ni moja ya wanakamati waliosimamia shughuri mzima ya bbq.
Kinyasi katibu wa kamati alisimama kidete kuhakikisha nyama inaliwa kwa ubora wa kioganiki.
Kulikuwa na wageni kutoka world wide, hapa ni Monalisa nguri wa Bongo movie Tanzania akiwa na Mtangazaji mahiri Tanzania wa enzi hizo Bi Rose Chitila na Lulu kutoka Maryland. Nyati Fc tutakuwa tunakuletea kila kilicho bora kwa mapendekezo ya kamati yake.
Kinyasi akipata ukodaki na akina Monalisa.
Baada ya BBQ mambo yaliamia Alamo hadi majogoo ni mwenda wa kula ngoma na DJ Mao na DJ Tito mambo yalikuwa moto. Unakosaje msimu wa tatu??????. Kwa Taswira zaidi nenda chini kiroho safi picha kama zote.
Monalisa, Rose na Lulu akiwa ng'ari ng'ari ndani ya Alamo.
James Lupemde mwenyekiti wa kamati akifurahia jambo na vijana wa Nyati Fc. |
No comments:
Post a Comment