ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 19, 2019

Mwanafunzi Kidato cha Nne Ajiua kwa Risasi

Ndugu Wanahabari, Tarehe 18.08.2019 muda wa saa 05:00hrs alfajiri katika Nyumba ya Shirika La Nyumba la Taifa iliyopo Plot namba 3 na 4, eneo la Soko Kuu la Arusha, Kata ya Kati katika Halmashauri ya Jiji la Arusha Faisal S/O Salimu Ibrahim (19), Mhindi, Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Arusha Meru alijiua kwa kujipiga risasi moja kichwani katika paji la uso katika chumba chake kwa kutumia bunduki aina ya Rifle Winchester inayomilikiwa na Baba yake aitwaye Salim S/O Ibrahim (56yrs) wanaoshi pamoja katika nyumba hiyo.

Chanzo cha tukio hili ni msongo wa mawazo uliotokana na matumizi ya madawa ya kulevya. Aidha mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi wa Daktari.

Natoa wito kwa Makampuni,Taasisi na Watu binafsi wanaomiliki silaha, kutumia silaha hizo kwa umakini mkubwa na pia kuzitunza sehemu sahihi ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kutokea endapo zitachukuliwa au kuibiwa na kutumika vibaya. Tutawafutia umiliki wale wote watakao zitumia silaha hizo kinyume na utaratibu uliowekwa na ambao watabainika kushindwa kuzitunza.

IMETOLEWA NA: ACP – JONATHAN SHANA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA

No comments: