ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 19, 2019

NAIBU WAZIRI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UMOJA WA ULAYA, NCHINI BOTSWANA

Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisalimiana na Mhe.Jan SADEK Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Botswana walipokutana kwa mazungumzo jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo baina yao yalijikita kwenye masuala mbalimbali yaliyojadiliwa kwenye Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Sambamba na hayo katika mazungumzo hayo Dkt. Ndumbaro aliendelea kumueleza Balozi Jan, juu ya umuhimu wa Umoja wa Ulaya kutekeleka wito alioutoa Mhe. Rais Magufuli wakati wa Mkutano wa SADC kuhusu kuiondolea nchi ya Zimbabwe vikwazo vya kiuchumi. Balozi Jan alikuwa nchini kuhudhuria Mkutano wa SADC
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza alipokutana kwa mazungumzo na Balozi Jan.
Mazungumzo yakiendelea
Mhe. Dkt. Ndumbaro akimsikiliza Balozi Jan walipokuna kwa mazungumzo jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Ndumbaro akisisitiza jambo alipokutana kwa mazungumzo na Balozi Jan.

No comments: