Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas amesema serikali itawafungulia kesi ya kuhujumu nchi watu wote watakaobainika kuihujumu serikali juu ya kukamatwa kwa ndege ya Tanzania nchini Afrika Kusini, pindi kesi iliyoplekea kukamatwa ndege hiyo itakapomalizika.
Akizungumza mjini Dodoma leo Jumamosi Dk Abbas amesema wapo Watanzania wanaishiriki kuihujumu Serikali kuhusu ndege hiyo, kwamba kuna siku uhujumu huo utawasaidia.
“Wapo wazawa wanaofanya mawili matatu kuhujumu nchi lakini niwaeleze tusubiri kesi iishe huko Afrika Kusini, tutawafungulia kesi ya kuhujumu nchi yetu.”
“Hakuna Nabii katika historia ya Manabii aliyewahi kuaminiwa kwa asilimia 100, hivyo huwezi kukubaliwa na watu wote, hata hii ndege inayoshikiliwa ikija Tanzania ipo siku wanaochukia watatumia usafiri huo kwenda Afrika Kusini kama sio wao basi watoto wao,” amesema Dk Abbas.
Jana Mawakili wanaoiwakilisha Tanzania katika kesi ya kuzuiwa ndege hiyo waliitaka mahakama Kuu ya Afrika Kusini kutupilia mbali zuio la kuzuia ndege ya shirika hilo ya Airbus A220-300, wakisema ilitolewa kimakosa.
No comments:
Post a Comment