ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 9, 2019

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI MAOMBI YA LISSU KUVULIWA UBUNGE

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es , imetupilia mbali maombi ya Tundu Lissu kupinga uamuzi wa Spika wa Bunge, Job Ndugai kumvua ubunge kwa maelezo kuwa alipaswa kuweka pingamizi dhidi ya uchaguzi na si kuomba mahakama ibatilishe uamuzi wa Spika.

Jaji Matupa amesema, hawezi kufanya maamuzi ya kufuta uamuzi wa Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa sababu ataingia kwenye mgogoro wa kikatiba na Mhimili wa Bunge.

Akiendelea kufafanua, Jaji Matupa amesema, endapo maombi hayo ya Lissu yakisikilizwa mpaka mwisho na Lissu akashinda kesi hiyo, Jimbo la Singida Mashariki litalazimika kuwa na Wabunge wawili (yaani Tundu Lissu na Miraji Mtaturu) kwa wakati mmoja.

No comments: