Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa sambamba na diwani wa kata ya Sadan wakati akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Ihanzutwa kwenye ziara ya kawaida jimboni
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa na diwani wa kata ya Sadan wakifurahia ujenzi wa ubora uliojengwa katika darasa la shule ya msingi Ihanzutwa kwa kupitia ufadhili wa TANAPA
Hili ni moja kati ya madarasa yaliyojengwa kwenye ubora wa hali ya juu kwa kupitia ufadhili wa TANAPA
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akifurahia jambo na watoto wa kijiji cha Ihanzutwa mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji hicho.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Wananchi wa Ihanzutwa
wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule ya
msingi Ihanzutwa na kukosekana kwa maji safi na salama katika kijiji hicho
hivyo wamemuomba mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini kusaidia kutatua kero hizo.
Wakizungumzana kwenye
mkutano wa hadhara,wananchi hao wamesema kuwa wanashukuru kwa ujenzi wa vyumba
vya madarasa lakini bado wanakabiliwa na ukarabati wa vyumba vitatu vya
madarasani katika shule hiyo.
“Sambamba nashukrani za
ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi za walimu na ukarabati wa vyumba
vitatu vya madarasa kwa fedha za serikali lakini bado tunaomba kusaidiwa
ukarabati wa vyumba vitatu vya madarasa ili kupunguza msongamano wa wanafunzi
darasani” walisema wananchi
Aidha wananchi wa kijiji cha
Ihanzutwa walisemakuwa wanakabiriwana uhaba wa maji kwa miaka mingi hali
inayosababisha wanawake kutumia muda mwingi kutafuta maji hivyo walimuomba
mbunge wa jimbo hilo kuwatafutia njia ya kutatua tatizo hilo
Akijibu maswali ya wananchi
mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa amesema kuwa ameipokea changamoto
hizo na atazifanyia kazi kwa kushirikianana wadaumbalimbali.
“Leo nikitoka hapa
nitaendeleza mazungumzo na TANAPA ili waendelee kutusaidia kama ambavyo
wametusaidia katika ujenzi wa madarasa na madarasa yaliyojengwa katika kijiji
hiki huwezi kuyapata kijiji chochote kile kwa kuwa wanaubora wa aina yake”
alisema Mgimwa
Aidha Mgimwa amesema kuwa
amewapata wadau ambao watasaidia kutatua kero ya maji kwakuchimba kisima kimoja
katika kijiji hiki cha Ihanzutwa.
“Tunamarafiki zetu wa Water
For Africa ambao wametuahidi kutuchimbia kisima kimoja kirefu kwa lengo la
kutatua changamoto hii ya maji katika kajiji hiki” alisema Mgimwa
No comments:
Post a Comment