NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi, Kija Magoma amesema Chama Cha
Mapinduzi (CCM), kilipoteza baadhi ya vijiji, vitongoji,mitaa, kata na
majimbo kwa fitna na uzembe wa wanachama wake na kuwataka wasirudie
makosa kwenye chaguzi zijazo.
Pia kimeonya wana CCM wanaojipitisha kwenye majimbo na kata wakifanya
kampeni za siri na kuanza kuchafuana na kuagiza majina yao
yaorodheshwe ili washughulikie kwa sababu wanakichafua Chama.
Magoma alitoa kauli hiyo jana jijini Mwanza, kwenye kongamano la
elimu, maadili,afya,mazingira, siasa na uchumi lililoandaliwa na
Wazazi Wilaya ya Nyamagana, kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa
mwaka huu.
Alisema mwaka 2014 na 2015 CCM ilishindwa kwenye baadhi ya maeneo kwa
sababu ya fitna, majungu, kusemana vibaya (kuchafuana) na uzembe wa
wanachama wake pindi uchaguzi unapokaribia, hivyo uchaguzi wa mwaka
huu wasirudie makosa hayo.
“Uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu ni wa kuonyesha dira ya
2020.Chama kwanza, mtu baadaye na tuache majungu, fitna,kuchafuana na
kutukanana, ikitokea hivyo hao tunaowachafua tukawapitisha itakuwa
fimbo ya kutuadhibu itakayotumiwa na wapinzani,”alisema Magoma.
Alisema wapo wana CCM kote nchini wanajipitisha kabla ya wakati
wakifanya kampeni za siri ili wapitishwe kugombea uongozi na kuonya
muda huo haujafika na wanaofanya hivyo wasidhani wako salama,wataanza
kuchukuliwa hatua wilayani kwa sababu wanaichafua CCM.
“Angalizo, serikali ya Rais John Magufuli si ya mchezo, wanaofanya
kampeni za ubunge na udiwani kabla ya wakati wanafahamika na taarifa
zao zipo mezani,na safari hii hakuna ujinga wa CCM kushindwa.Hapa
Nyamagana kuna watu wanamvuruga mbunge ili kumuondoa, muda bado
haujaisha.Wabunge na madiwani waheshimiwe ,waachwe wafanye
kazi,”alisistiza Magoma.
Akizungumzia utaekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi alisema imetekelezwa
ndani ya miaka mitatu na nusu ya uongozi wa Rais Magufuli kutokana na
ualidifu na uzalendo wake wa kuhakikisha nchi inapata maendeleo ya
kweli aliyoahidi wakati wa kampeni.
Alisema Rais Dk. Magufuli kwa aliyoyafanya ni dhahiri ameshaifanyia
CCM kampeni kwa asilimia 80 hata kabla ya uchaguzi, hivyo ni jukumu la
wana CCM kutafuta takwimu na kuwaeleza wananchi yaliyofanyika kwa
sababu hakuna mwingine wa kuyasema lakini wakikaa kimya ni kutomtendea
haki.
“JPM anastahili pongezi kwa namna alivyotekeleza ilani ya CCM katika
muda mchache,amejenga miundombinu ya barabara km 12,885, fly over na
Ubongo Interchange kwa bilioni 247,litajengwa daraja la Kigongo-Busisi
(Milioni 700),amenunua ndege sita tayari,amelipa madeni ya watumishi
sh. bilioni 595.2,”alisema Magoma.
Aliongeza kuwa amefanikiwa kujenga vituo vya afya 118, zahanati 522,
hospitali 67 za wilaya ambapo 34 zimekamilika,ujenzi wa majengo ya
ukaguzi wa elimu kote nchini kwa bilioni 15.2, umeme umeunganishwa
kwenye vijiji 7,100, ujenzi wa mradi wa umeme Stiglers kwa Trilioni
6.5, Reli ya kisasa (SGR) kwa Trilioni 7 kwa fedha za ndani.
“Anataka Tanzania iwe nchi ya mfano ambapo bajeti ya mwaka huu ni
Trilioni 33.11 kati ya hizo trilioni 12.15 za maendeleo, mikopo
trilioni 2.52, bajeti ya dawa sh. milioni 415 (2019/2020) na elimu
bilioni 450,”alisema Naibu Katibu Mkuu huyo wa Wazazi na kuhoji
,tulichelewa wapi kumpata Rais wa aina hii mwenye maono makubwa na
nchi, uchumi unapanda.sssss
No comments:
Post a Comment