ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 9, 2019

PSPTB YATOA ONYO KWA WACHELEWESHAJI WA MIRADI

 Mwezeshaji Aziz M. Kilonge akitoa mafunzo kwa wataalamu wa ununuzi na ugavi waliofika kwenye mazunzo hayo yaliyoandaliwa na Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi nchini (PSPTB) yanayofanyika kwa siku tano katika ukumbi wa Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi wakifuatilia mada wakati wa mafunzo ya Siku tano yaliyoandaliwa na Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi nchini (PSPTB).



Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi nchini PSPTB wamewataka wataalamu wa ununuzi na ugavi nchini kusimamia na kutoa ushauri wa manunuzi ili kutopoteza fedha za walipa kodi pamoja na serikali hasa katika miradi ya kimkakati maana hatua kali zitachukuliwa ikiwemo kufutiwa usajili.

Akifungua mafunzo ya siku tano kwa wataalamu wa ununuzi na ugavi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Umma (PSPTB), Godfred Mbanyi amesema ya wataalam hao wameonekana kusababisha ucheleweshaji mkubwa wa miradi na upotevu wa fedha kwa kutotoa ushauri na kusimamia vizuri utekelezwaji wa miradi hiyo.

Amesema kuwa lazima wataalamu hao wanaosimamia masuala ya ununuzi na ugavi lazima wafanye kazi kwa kuzingatia kanuni pamoja na kutoa maoni pindi wanaposhauri michakato ya ununuzi na pindi maoni yao yanapopingwa watoe taarifa ili kuokoa miradi ambayo serikali imeelekeza kwa wananchi.

Vilevile amewahimiza wataalamu hao kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa wakati na sio kusubiri malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya serikali ambayo imetekeleza kila kitu ila watendaji ndio wanaokwamisha mlolongo mzima wa utekelezaji.

Mbanyi amesema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Joseph Magufuli inafanya kazi kwa vitendo zaidi hivyo watendaji lazima waendane na kasi hiyo ili kujenga Tanzania ya viwanda na kulipeleka taifa kwenye uchumi wa kati.

No comments: