ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 7, 2019

SHUKURANI ZA DHATI

Familia ya Andrew Tandau na Jacqueline Korassa Tandau tunapenda kutoa shukrani nyingi sana na za kipekee kwa Wana DMV wote,Ndugu,Jamaa na Marafiki,Viongozi wa Dini na Jumuiya kwa ujumla kwa kujitoa kwa hali na mali katika kufanikisha shughuli nzima ya kumsafirisha Mama yetu Mpendwa Cecilia Joseph Korassa aliyefariki siku ya Alhamisi tarehe 22 August ,2019 akiwa hapa Washington DC na kuzikwa siku ya Alhamisi September 5 ,2019 nyumbani kwake Tanzania..

Shukrani za kipekee ziwaendee kanisa la Swahili Lutheran Church Ambalo lipo hapa Rockville,Maryland (Mchungaji John Mbatta na Muinjilisti Mama Eilen Mushi wakiwemo Wanakwaya na Waumini wote)Kwa kujitolea kuja kumwombea Mama bila kuchoka toka akiwa hospitali na hata alipokuwa nyumbani na kumpa Mama nafasi ya kushiriki Chakula cha Bwana(Sacramental), Upendo mliotuonyesha ni mkubwa mno, Tunawashukuru Sana Sana Sana.

Tunapenda kutoa Shukrani pia kwa Mchungaji Dr Nicku/ Moddy wa Kanisa la Bethel World Outreach Church na Father/ Padre Honest Munishi kutoka kanisa la St Edward Roman Catholic Church la Baltimore Kwa kujitolea kushiriki na Sisi katika Misa ya kumwaga Mama,

Shukrani zingine kwa kanisa la The Way of the Cross Gospel Minisitries Kwa kujitolea kuja kutufariji nyumbani wakati wa msiba...

Pia bila kusahau Makanisa mengine yote na Prayer line groups za Umoja Church, Texas zilizokuwa zinamwombea Mama usiku na mchana.

Shukran pia ziwaendee Kamati nzima ya msiba kwakusimamia maandalizi yote na kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri na salama kuanziaa mwanzo mpaka mwisho.

Shukrani za kipekee ziwaendee ndugu jamaa na marafiki waliotoka out of town na nje ya Nchi ili tu kuweza kuja kuwa Pamoja na sisi katika kipindi hiki kigumu..

Tunawashukuruni Sana Sana Wote Kwa Upendo wenu na Kwa michango yenu yote mliotoa.

Hatuna cha kuwalipa Bali tunasema Asante na Mwenyezi Mungu Awabarikini wote na kuwazidishiaa pale mlipotoa..

Upendo mliotuonyesha ni mkubwa mno..Tunasema Asante na Mungu Aendelee kutuwezeshaa wote kuuendeleza na kudumisha Upendo huu.

***BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE MILELE..
AMEN***

No comments: