Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Israel Balozi Job Daud Masima wakati wakizungumza na ujumbe wa Wakurugenzi 6 wa Mashav wa Wizara ya Mambo ya nje ya Israel katika mkutano wa kazi uliofanyika katika Ofisi za wizara ya Mambo ya nje ya Israel iliyopo mtaa namba 9 Yitzhak Rabin Jijini Jerusalem nchini Israel, leo tarehe 5 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) na Balozi wa Tanzania nchini Israel Balozi Job Daud Masima wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Wakurugenzi 6 wa Mashav wa Wizara ya Mambo ya nje ya Israel mara baada ya mkutano wa kazi uliofanyika katika Ofisi za wizara ya Mambo ya nje ya Israel iliyopo mtaa namba 9 Yitzhak Rabin Jijini Jerusalem nchini Israel, leo tarehe 5 Septemba 2019.
Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wakizungumza na ujumbe wa Wakurugenzi 6 wa Mashav wa Wizara ya Mambo ya nje ya Israel katika mkutano wa kazi uliofanyika katika Ofisi za wizara ya Mambo ya nje ya Israel iliyopo mtaa namba 9 Yitzhak Rabin Jijini Jerusalem nchini Israel, leo tarehe 5 Septemba 2019.
Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Israel Balozi Job Daud Masima wakisindikizwa na Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Ushirikiano wa mambo ya nje nchini Israel Ndg Yuval Fuchs mara baada ya mkutano wa kazi uliofanyika katika Ofisi za wizara ya Mambo ya nje ya Israel iliyopo mtaa namba 9 Yitzhak Rabin Jijini Jerusalem nchini Israel, leo tarehe 5 Septemba 2019.
Na Mathias Canal, Jerusalem-Israel
Waziri wa Kilimo wa
Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 5 Septemba 2019 amekutana na
kufanya mazungumzo na ujumbe wa Wakurugenzi 6 wa Mashav wa Wizara ya Mambo ya nje ya Israel.
Katika mkutano huo wa
kazi uliofanyika katika Ofisi za wizara ya Mambo ya nje ya Israel iliyopo mtaa
namba 9 Yitzhak Rabin Jijini Jerusalem nchini Israel, Waziri wa Kilimo
amewasilisha mambo mbalimbali kuhusu sekta ya kilimo ikiwemo ufuatiliaji wa
utekelezaji wake.
Mhe Hasunga
ameishukuru serikali ya Israel kwa kukubali ombi la Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli la kuongeza idadi ya wanafunzi wanaoshiriki
mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies katika kipindi cha mwaka mmoja kutoka 45
ambapo imefikia idadi ya wanafunzi 100.
Katika kikao hicho Waziri
Hasunga amewakumbusha Mabalozi hao sita kuhusu ombi la Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli la kuongezwa idadi ya
wananfunzi kufikia idadi ya wanafunzi 300.
Mhe Hasunga amesema
kuwa Balozi huyo amepongeza kwa dhati na kuunga mkono juhudi za serikali ya
Tanzania inayoongozwa na Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwani ni serikali ya
vitendo na uwajibikaji hivyo wapo tayari kuhakikisha kuwa ushirikiano
unaboreshwa baina ya nchi hizo mbili.
Kikao hicho pia
kimejadili kwa kina namna ya kuboresha zaidi mahusiano baina ya nchi ya
Tanzania na Israel hususani katika kuimarisha ushirikiano kwenye nyanja za utafiti,
uongezaji thamani wa mazao, na namna ya kuongeza ukubwa wa mashamba na kilimo
tija.
Pia, Mhe Hasunga
amewasilisha ombi la kupata kampuni mbalimbali za nchini Israel ili kuzuru
Tanzania na kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji.
“Tukipata kampuni za
kuisaidia Tanzania kwenye maswala ya kilimo cha umwagiliaji tutakuwa na fursa
ya kubadili kilimo chetu kutoka kwenye kilimo cha kutegemea mvua na hatimaye
kuingia katika kilimo cha umwagiliaji” Alisisitiza Mhe Hasunga na kuongeza kuwa
Serikali ya Israel
imekubali kufikiria kuongeza idadi ya vijana kutoka Tanzania wanaozuru Israel
kwa ajili ya kujifunza ambapo pia wataongeza uwezekano wa wataalamu mbalimbali
wakiwemo maafisa ugani nchini Tanzania kuzuru Israel kwa ajili ya kujengewa
uwezo katika utendaji.
Kwa upande wake Naibu
Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Ushirikiano wa mambo ya nje nchini Israel
Ndg Yuval Fuchs amesema kuwa serikali ya Israel imeridhia maombi ya Waziri wa
Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga na kusema kuwa Israel ipo tayari
kushirikiana na Tanzania ili kuboresha sekta ya kilimo kutoka kwenye kilimo cha
kujikimu kuwa kilimo cha kibiashara
Vilevile amesema kuwa
atazishawishi kampuni mbalimbali kuwekeza nchini Tanzania kwa ushirikiano mzuri
na serikali kwani Tanzania kuna ardhi nzuri yenye rutuba kwa ajili ya kilimo.
Kadhalika amempongeza
Waziri Hasunga kwa kutembelea nchini Israel kwa ajili ya ziara ya kikazi ambapo
amesema kuwa kumekuwa na kikao muhimu kilichojadili namna ya kuboresha kilimo
nchini Tanzania.
Kadhalika,
Balozi wa Tanzania nchini Israel Balozi Job Daud Masima amesema kuwa kikao cha
Waziri wa Kilimo ni muendelezo wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo nchini Israel ambapo
ameongeza kuwa kikao hicho kimetoa taswira ya kutafakari kwa pamoja kuona namna
mafunzo hayo yanavyowasaidia vijana wa kitanzania.
Amesema
Waziri Hasunga amekutana na ujumbe wa mabalozi 6 pamoja na wasaidizi wake
wanaohusika na maswala ya Afrika Mashariki, kikao hicho kimetoa heshima kubwa
kwa serikali ya Tanzania ambapo vijana 100 watapokelewa nchini Israel na waziri
Hasunga leo tarehe 5 Septemba 2019.
Naye Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya agrostudies Ndg Yaron Tamir amesema kuwa wanafunzi walioshiriki
mafunzo hayo kutoka Tanzania wametoa ushirikiano mzuri hivyo mafunzo hayo waliyoyapata
wanapaswa kuyaendeleza ili kuboresha kilimo nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment