TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUAPISHWA RASMI KWA MFALME MPYA WA JAPAN
Dodoma, 19
Oktoba 2019
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt. (Mst) George Mkuchika (Mb.) atahudhuria
sherehe za kuapishwa na kutambulishwa kwenye Jumuiya ya Kimataifa kwa Mfalme
Naruhito wa Japan zitakazofanyika jijini Tokyo tarehe 22 Oktoba 2019.
Mhe.
Mkuchika anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambaye
aliakwa katika sherehe hizo na Waziri Mkuu wa Japan, Mhe. Shinzo Abe.
Kwa
mujibu wa katiba na sheria za Kifalme za Japan, Mfalme Naruhito amerithi kiti
cha Baba yake, Mfalme Akihito ambaye alitangaza kujiuzulu rasmi nafasi yake
tarehe 30 Aprili 2019 kutokana na umri wake kuwa mkubwa sanjari na kusumbuliwa
na matatizo ya kiafya. Mfalme Naruhito alichukua madaraka hayo tarehe 1 Mei
2019.
Mhe.
Mkuchika na ujumbe wake wanatarajia kuondoka nchini tarehe 19 Oktoba 2019 na
kurejea tarehe 24 Oktoba 2019.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki,
|
No comments:
Post a Comment