Kaimu meneja mkuu wa kampuni ya ranchi za taifa NARCO profesa Philemoni Nyangi Wambura atafikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Bukoba leo tarehe 30 okitoba mwaka huu kwa tuhuma za rushwa matumizi mabaya ya ofisi ubadhilifu na uhujumu uchum kinyume na sheria namba 11 ya mwaka 2007 ya kuzuia na kupambana na Rushwa
Hayo yamebainishwa na mkuu wa takukuru mkoa wa kagera JOHN JOSEPH wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake
Bw.joseph amesema kuwa Takukuru mkoa wa Kagera ikiwa katika utekelezaji wa majukumu yake mnamo Septemba 23 mwaka huu walipata taarifa kutoka katika vyanzo vyake kuwa kaimu meneja wa NARCO profesa wambura amekuwa akijihusisha na na vitendo vya rushwa ikiwa nikuomba na kupokea rushwa kutoka kwa baadhi ya wafugaji wenye uhitaji wa vitalu vya kufugia ng”ombe pamoja nawafugaji wanaotaka kuhuisha mikataba ya yao ya awali.
Akizungumza bw.Joseph amesema kuwa taarifa zinasema kuwa tarehe 3/1/2018 profesa Wambura kaimu meneja mkuu wa NARCO mkoa wa kagera alipokea jumla ya milioni 12 kutoka kwa mtu jina limeifadhiwa aliyeitaji kupewa kitalu kwa ajili yakufanya shughuli zake za ufugaji.
Pamoja na tukio hilo taasisi ya kuzuia na kupambana narushwa TAKUKURU mkoa wa Kagera mnamo tarehe 25/10/2019 iliwafikisha mahakamani watu wengine wanne ambao ni bw.Stansilaus Kato mwenyekiti wakamati ya ujenzi wa shule ya sekondari kashenye aliye funguliwa shauri jinai namba 226 la mwaka 2019 kwa makosa ya kughushi nyaraka nakujipatia madaraka asiyokuwanayo nakuwasilisha nyaraka za uongo kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya misenyi kwa lengo la kujipatia shilingi milioni tano laki saba elfu themanini na nne mia saba na arobaini.
Nawatu wengine waliofikishwa mahakamani na bw.Richard Machumi Kavorogo mwenyekiti wa kijiji cha omkalinzi ,bw.Joseph Desekahino Nzeye ofisa mtendaji wa kijiji omkalinzi na bw.Onesmo Mabadiliko Tiara aliyekuwa mwenyekiti wa kamati za vocher za pembejeo wa kata ya muganza halmashauri ya wilaya Ngara watatu hao wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ngara kujibu mashitaka yanayo wakabiri.
Vilevile bw.JOSEPH amesema nivyema wananchi waishio mkoa wa kagera waendelee kushirikiana na TAKUKURU pamoja na kutoa taarifa ili kuwabaini wala rushwa na mafisadi wanaotumia vibaya madaraka na maliza umma,kadhalika bw Joseph amesema kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa wananchi watakao shuhudia vitendo vya rushwa wasisite kutoa taarifa TAKUKURU kwa kupiga simu namba 113 bure
No comments:
Post a Comment