Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Tombe Magufuli akiongea kwa simu na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro na kumuagiza kumsimamisha kazi mara moja Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Sumbawanga ACP Polycarp Urio kwa kutowasilisha taarifa kwa Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa maelekezo ya Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Kangi Lugola ambaye hivi karibuni aliagiza kuhamishwa kituo cha kazi askari polisi Tisa waliokuwa wakijihusisha na vitendo vya rushwa na kuwabambikizia kesi wananchi. Mhe. Rais alitoa matatizo hayo alipotembelea Kituo cha Polisi cha Laela mara baada ya kuzindua rasmi Barabara ya Tunduma-Laela-Sumbawanga yenye urefu wa kilometa 223.2 ambayo ni sehemu ya barabara kuu katika ushoroba wa Magharibi unaoanzia Tunduma-Mpanda-Kigoma-Nyakanazi wenye urefu wa kilometa 1,286. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment