ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 7, 2019

TCRA YAWAJENGEA UELEWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM JUU YA USAJILI WA LAINI ZA SIMU KWA MFUMO WA ALAMA ZA VIDOLE.

Mkuu wa wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Daqqaro akizungumza na watu wenye mahitaji maalumu, kuilia kwake ni Philipo Meli Mwenyekiti wa watu wasioona mkoa wa Arusha, kushoto kwake ni Mhandisi Imelda Salum Mkuu wa kanda ya kaskazini Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA na wa kwanza kulia ni Katibu wa chama cha Viziwi Tanzania tawi la Arusha.
MHANDISI Imelda Salum ni Mkuu wa kanda ya kaskazini (TCRA akizungumza na watu wenye mahitaji maalum Viziwi na watu walemavu wasioona
Julius Felix Mwanasayansi wa Masafa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini kanda ya Kaskazini TCRA ,wengine ni washiriki wa semina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka hiyo kwaajili ya kuwajengea uelewa juu ya usajili wa laini za simu kwa kutumia mfumo wa alama za vidole.
Jan Kaaya ni Mhandisi Mwanadamizi wa Masafa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA).Picha na Vero Ignatus
Baadhi ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA)Viziwi na walemavu wasioona uliofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Arusha.
MHANDISI Imelda Salum ni Mkuu wa kanda ya kaskazini (TCRA akizungumza na watu wenye mahitaji maalum Viziwi na watu walemavu wasioona katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA)Viziwi na walemavu wasioona uliofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Arusha.
Baadhi ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA)Viziwi na walemavu wasioona uliofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Arusha.
Mhandisi Imelda Salum Mkuu wa kanda ya kaskazini Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA akizungumza katika uzinduzi wa semina hiyo ya siku moja ya wadau wa mawasiliano ,kutoka makundi mawili Viziwi na walemavu wa kutoona.
Mmmoja wawakalmani wa lugha ya alama wakiwasaidia watu wenye mahitaji maalumu kuelewa kile kinachoendelea katika mkutano huo wa siku moja ulioandaliwa na TCRA Mkoani Arusha.
Mmmoja wawakalmani wa lugha ya alama wakiwasaidia watu wenye mahitaji maalumu kuelewa kile kinachoendelea katika mkutano huo wasiku moja ulioandaliwa na TCRA Mkoani Arusha.
Baadhi ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA)Viziwi na walemavu wasioona.
Mmoja wa wakalimani wa lugha ya aklama akisaidia ujumbe ufike kwa waandaaji wa semina ya watu wenye mahitaji maalum (TCRA).(Picha na Vero Ignatus)
Na Vero Ignatus, Arusha
Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kanda ya kaskazini imefanya mkutano wa siku moja na wadau wa mawasiliano wenyenye mahitaji maalumu, wakiwa katika makundi mawili Viziwi na walemavu wa kutokuona.
Lengo haswa la mkutano huo ni kutoa uelewa kwa watu wenye mahitaji maalum, kuhusu zoezi la usajili wa laini za simu kwa njia ya mfumo wa alama za vidole ,pia kuangalia changamoto mbalimbali walizonazo katika huduma za Mawasiliano
Gabriel Daqqaro ni mkuu wa wilaya ya Arusha amesema kuwa semina hiyo itasaidia ,ukizingatia kwasasa kuna changamoto nyingi za mitandao japo kuwa zipo faida zake kama vile kupashana habari,kuelimisha,kuburudisha na kukataza yale mambo mabaya katika jamii katika maendeleo yanayokwenda kwa kasi.
Amesema kuna makosa ya uhalifu wa kimtandao ,watu wasiowaaminifu wanaotuma jumbe za kulaghai wa wananchi,kwasababu hiyo serikali imeelekeza laini zote za simu zisajiliwe kwa alama za vidole ,hivyo ameipongeza TCRA kwa kuona watu wenye ulemavu kuwa ni sehemu ya jamii.
“Watu hawa wenye mahitaji maalumu wananchwa mara nyingine kutokana na baadhi ya watu kudhania kwa mawazo yao hasi kwamba ulemavu ni hasara,niseme hujafa huijaumbika,nisisitize hebu tubebane tonane tupo sawa.
Daqqaro amesema serikali ya awamu ya tano imeona hilo, ndipo ikaona watu wenye mahitaji maalum ,walikuwa hawajajumuishwa katika kunufaika na zile 10% za mapato ya ndani ,kuanzia mwaka 2018 imetoa maelekezo kwamba na wenyewe ni miongoni mwa kundi linalotakiwa kunufaika ,ambapo halmashauri zote zimeelekezwa hivyo .
Amesema ni muhimu kusajili line za simu ili kuepusha makosa ya uhalifu wa kimtandao, matapeli wanao tuma jumbne
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo mkuu wa wilaya ya Arusha amesema serikali serikali iliagiza kuwa 10%za mapato nao watu wenye ulemavu wanufaikike na mapato ya ndani iliagiza laini zote za simu zisajiliwe kwa mfumo wa alama za vidole hivyo watu wenye uhitaji maalumu nao ni sehemu ya jamii.
MHANDISI Imelda Salum ni Mkuu wa kanda ya kaskazini(TCRA) amesema kuwa Mamlaka hiyo imeamua kwasababu wao nao ni sehemu ya jamii ,na pia wanatumia huduma ya mawasiliano hivyo .wanahaki ya kupata taarifa mbalimbali,mafunzo.
“Tunafahamu kwa namna walivyo wenzetu wana changamoto mbalimbali yumkini kuna wengine hawawezi kupata taarifa kwa wakati ,lakini kwa wenzetu wa kwa wasiosikia taarifa kwa taarifa zinazopelekwa kwa jamii kwa njia ya radio,televisheni,asiyeona hawezi kuona kwenye televisheni,halikadhalika asiyesikia vileviel”
TCRA imesema kwa kuona umuhimu wa kundi hilo wameamua kuwashirikisha Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA)ili waweze kutoa huduma kwa watu hao wenye mahitaji maalum
Mkuu huyo wa kanda ya amesema Swala la usiri na faragha kwa watu wasioona bado limekuwa ni tatizo ,mawasiliano yao yanaweza kutatuliwa tu endapo kuna vifaa maalumu ambavyo wanaweza kuvitumia zikiwemo simu za mkononi ,pale mtu anaposoma ujumbe aweze kusikia sauti ujumbe unasemaje.

''Ila mamlaka ya mawasiliano tunajitahidi kuona ni kwa namna gani tunaweza kuwasaidia ,kwa wenzetu wasioona tunawapa taarifa mbalimbali kupitia vitabu ambavyo vimechapiushwa kwa zile alama zao maalum.''

Ameainisha kuwa kila mmoja aone umuhimu wa kujisajili ni kwani watakaposajili kutumia alama za vidole taarifa zao zinafahamika ,sambamba na kuimarusha usalama wanapotumia mawasiliano.

Ametoa wito kwa jamii kulitilia uzito swala hili la kusajili laini,na kwa wale ambao hawajapata kitambulisho cha NIDA,Mamlaka husika itawasaidia kupata namba zao,sambamba na wale ambao hawajajiandikisha NIDA wapo tayari kwaajili ya kuwasaidi ili wajiandikishe wapate kitambuluisho cha taifa.
Philipo Meli ni mwenyekiti wa wasioona mkoani Arusha amesema wanaishukuru TCRA kwa kuwathamini na kuwapatia semina hiyo ya kuwajengea utaalamu na kuwapatia vitabu vya nykta nundu kwaajili ya kujisomea na kupata uelewa kuhusiana na mamlaka hiyo ya mawasiliano.
Amesema katika mawasiliano watu wasioona changamoto kubwa ni mtu wa kuwasomea ujumbe lazima awepo,hakuna usiri,tunaomba serikali itusaidie uwepo wa simu ,ambazo tunaweza kusoma ujumbe kwa kusikia sauti ,na iwe katika lugha ya kiswahili ambapo itaweza kuondoa utegemezi kwa kiwango kikubwa.
"Changamoto kubwa mtu anakutumia ujumbe hata kama unataka uwe wa siri,inashindikana mpaka utafute mtu mwaninifu aweze kukusomea ujumbe wako,hiyo ndiyo changamoto inayotupata sisi watu tusioona.''Alisema Philipo

No comments: