ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 24, 2019

TIMU YA YOUNG STARS MABINGWA WA KOMBE LA FA MKOA WA IRINGA

Mbunge wa jimbo la Kilolo Vennance Mwamoto pamoja mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava wakimkabidhi kombe la ubingwa wa FA mkoa wa Iringa nahodha wa timu ya Young Stars baada ya kuwafunga timu ya mbega mwekundu goli 5-1 mchezo uliochezwa katika uwanja wa mkwawa
 Mbunge wa jimbo la Kilolo Vennance Mwamoto pamoja mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava wakimkabidhi kombe la ushindi wa pili wa FA mkoa wa Iringa nahodha wa timu ya mbega mwekundu baada ya kufungwa goli 5-1 na timu ya Young Stars kwenye mchezo uliochezwa katika uwanja wa mkwawa
 
Mbunge wa jimbo la Kilolo Vennance Mwamoto alitoa pia zawadi ya kitamba cha unahodha kwa timu ya Young stars

Na Fredy Mgunda,Iringa.

TIMU ya Soka ya Young Stars imefanikiwa kuwa mabingwa wa kombe la FA mkoa wa Iringa baada ya kuibuka na ushindi ushindi wa magoli 5-1 dhidi ya Mbega Wekundu fc ya wilaya ya kilolo.

Katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa chuo kikuu cha Mkwawa timu ya Young Stars walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 13 kupitia kwa mshambuliaji hatari Zacharia Mwipopo.

Mchezo huo uliokuwa wa kukamiana mwanzo mwisho huku baadhi ya wachezaji wakionyesha ufundi mwingi wa kuchezea mpira hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Young Stars walikuwa wakiongoza bao 1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa kila timu kutaka kuonyesha kuwa hawajabahatisha kufika fainali ya FA Mkoa wa Iringa kwa Mbega wekundu kusawazisha goli kwa njia ya penati iliyopigwa na Gibo Laurence dakika ya 51 kipindi cha pili,lakini timu ya Mbega Mwekundu dakika  61mchezaji wao Nick King akipata kadi nyekundu nakuifanya timu hiyo kuwa pungufu na vua ya magoli ilipo waangukia timu hiyo

Baada ya kadi nyekundu waliyopata timu ya Mbega Mwekundu,timu ya Young Stars waliongeza mashambuli kwa kasi kubwa na kuanza kushusha vua ya magoli kwa timu pinzani ikiwa dakika ya 62 mchezaji Johnson Mwakatumbula aliipatia goli timu yake huku  Zacharia Mwipopo akirudi tena kambani 72 na shughuli ilimaliziwa na mchezaji  Maulid Chitonela alifunga magoli mawili katika dakika ya 84' 86 hadi mwisho wa mchezo  Young Star 5-1 Mbega Wekundu

Baada ya mchezo huo mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava aliwataka wachezaji wa timu zote mbili kucheza kwa nidhamu ya juu kwa kuwa mpira wa miguu ndio unataka hiyo.

Timu ya Mbega Mwekundu leo hii hamjaonyesha nidhamu kwenye mechi hii ya leo hiyo mnatakiwa kulinda nidhamu yenu ili muwezekufika mbali kisoka.

Naye mbunge wa jimbo la Kilolo Vennance Mwamoto amewapongeza wachezaji wa timu zote mbili kwa mchezo huo na kuwaomba waendelee kulinda nafasi yenu katika soka

No comments: