MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Msichana Uwezo na mwanaharakati wa haki za mtoto wa kike nchini,
Rebeca Gyumi, ameshinda rufaa iliyokatwa na Serikali katika Mahakama ya Rufaa Tanzania dhidi ya hukumu ya Mahakama Kuu Dar es Salaam iliyopinga ndoa za utotoni.Hukumu hiyo ilitolewa jana Jumatano, Oktoba 23, 2019, ambapo mahakama ilitengua kipengele cha sheria Sheria ya Ndoa inayoruhusu mtoto mwenye umri wa miaka 14 (aliye chini ya umri miaka 18) kuolewa. Ushindi huo sasa unawapa nguvu ya kwenda bungeni kurekebisha Sheria hiyo.
“Leo ni siku muhimu kwa sababu imeweza kuthibitisha kile ambacho Mahakama Kuu ilikisema kuhusiana na umri wa chini wa kuoa na kuolewa kwa mtoto wa kike na wa kiume, kwetu sisi kama shirika ni ushindi mkubwa.
GPL
No comments:
Post a Comment