Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bi. Coletha Shayo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Gehandu kuhusu umuhimu wa wanaume kushirikiana na wanawake katika kuzalisha chakula wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara.
Katibu Tawala Wilaya ya Hanang Bw Paulo Bura akizungumza na wananchi wa kijiji cha Gehandu na kusisitiza wanaume kutouza chakula na kuicha familia ikiwa na njaa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, na Watoto Bw. Abel Palapala akitoa elimu kwa wanakijiji wa Gehandu kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi kwa wananchi wanaoishi vijijini wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, na Watoto Bi. Silvia Siriwa akieleza uhusisano ulipo kati ya uzalishaji na mwanamke kwa wananchi wanaoishi vijijini wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara. Pix 5 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Gehandu wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
Wanaume nchini Tanzania wameaswa kuwasaidia wanawake katika shughuli
za maendeleo hasa katika uzalishaji wa chakula katika kaya ili
kuondokana na upungufu wa chakula katika familia.
Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bi.
Coletha Shayo katika Kijiji cha Gehandu kilichopo katika Wilaya ya
Hanang mkoani Manyara wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani
ikiwa na kauli mbiu isemayo " Lishe Bora kwa Ulimwengu usio na njaa"
Bi. Coletha ameongeza kuwa wanaume ni nguzo muhimu kwa familia na
kuwataka wanaume kutelekeza familia zao wakati wa uhaba wa chakula
bali kujipanga pamoja kwa kuweka chakula cha akiba.
Amewataka wanawake na Wanaume wa Kijiji cha Gehandu kuchangamkia fursa
zilizopo ikiwemo uwepo wa ardhi nzuri na wataalam wa kilimo na mifugo
ili kulima kilimo cha bora na kuwa na ufugaji wa kisasa.
Aidha amewataka wananchi hao kushirikiana katika kuhakikisha wanakuwa
na mafanikio katika shughuli za kilimo na ufugaji ili kusaidia kuleta
maendeleo katika kijiji chao.
"Niwatake wananchi wa kijiji hiki kuzingatia utunzaji wa chakula hasa
suala la lise bora katika familia ili kuondokana na tatizo la udumavu
kwa Watoto" alisisitiza Bi. Coletha
Naye Katibu Tawala Wilaya ya Hanang Bw Paulo Bura amesisitiza wanaume
kushirikiana na wanawake kuzalisha chakula kwa ajili ya chakula na
kuuza ili kujenga uchumi wa kaya na taifa kwa ujumla.
Ameongeza kuwa wanaume walio wengi wamekuwa wakiona fahari kuwa na
mifugo mingi huku familia zao zikiwa katika hali duni hivyo amewataka
kuitumia mifugo kuwasaidia kupata chakula, kununua mashamba na
kusomesha watoto.
"Kuna mila za kuwa na mifugo mingi katika jamii nyingi za wafugaji
huku wakikosa huduma nyingine kama chakula elimu na afya tusiifanye
mifugo fahari itusaidie katika kuendeleza familia zetu" alisema Bw.
Bura
Akielezea mikakati ya Wizara yenye dhamana kwa wanawake Mratibu wa
Maadhimisho kutoka Wizara husika Bi. Silyvia Siriwa amesema Wizara
imejikita katika utoaji wa elimu kwa wanawake itakayowasaidia
kujikwamua kiuchumi na pia kuondokana na vitendo vya ukatili katika
jamii.
"Mwanamke akiwezeshwa kiuchumi katika jamii anaondokana na vitendo
ukatili wa kijinsia na kuisaidia jamii inayowazunguka" alisisitiza Bi.
Silyvia
Naye Mkazi wa Kijiji cha Gehandu Bi. Pili Mussa amesema kuwa wanaume
wamekuwa wakiuza mazao bila kuwashirikisha na kusababisha njaa katika
familia nyingi na hata kuzikimbia familia zao wakati wa uhaba wa
chakula kwa kigezo cha kwenda kutafuta maisha.
Kwa upande Mkazi wa Kijiji cha Gehandu Bw. Samwel Arajiga amesema kuwa
baadhi ya wanaume wamekuwasababu ya kuleta njaa katika familia kwa
kuuza mazao yote na kutumia pesa kunywe pombe hivyo ameomba elimu
zaidi kutolewa kuhusu umuhimu wa kutunza chakula katika familia.
Amesisitiza utolewaji wa elimu ya kilimo bora na lishe bora kwa
wananchi wa vijijini ili kuondokana na tatizo la udamavu kwa
kuzingatia ulaji bora kwa watoto na familia zao.
No comments:
Post a Comment