ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 14, 2019

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA PSSSF HOSEAH KASHIMBA

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hoseah Kashimba Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma Novemba 13, 2019. Bw. Kashimba alifanya mazungumzo na Mhe. Spika ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake kubadilishana mawazo ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero mbalimbali kutoka kwa waheshimiwa wabunge kuhusu huduma za Mfuko.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw.. Hoseah Kashimba alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma, Kwa ziara ya kikazi ya kusikiliza kero za Wabunge
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akikabidhiwa kijarida cheche taarifa mbalimbaliz a shughuli za Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bw. Hoseah Kashimba alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma, Kwa ziara ya kikazi ya kusikiliza kero za Wabunge, Kulia ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi. 9PICHA NA OFISI YA BUNGE).

No comments: