Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Bw. Gervace Stephano Makoye katibu wa Ccm wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita alipomtembelea ili kumjulia hali nyumbani kwake Chato. Disemba 22, 2019. Bw. Makoye aliyewahi kuwa katibu wa Mhe. Magufuli kwa miaka 10 wakati akiwa Mbunge wa Chato anaendelea na matibabu nyumbani kwake katika Mtaa wa Kalema Chato Mjini Mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali na Wanafamilia pamoja na waombolezaji wengine nyumbani kwa marehemu Mzee Atanasi Masansa Mnaku aliyefariki Dunia Desemba 25, 2019 Wilayani Chato Mkoa wa Geita wakati alipokwenda kuwapa pole wafiwa kwa kuondokewa na Mpendwa wao leo Desemba 27, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Mzee Atanasi Masansa Mnaku aliyefariki Dunia Desemba 25, 2019 Wilayani Chato Mkoa wa Geita wakati alipokwenda kuwapa pole wafiwa kwa kuondokewa na Mpendwa wao leo Desemba 27, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kusajili Laini ya simu kwa njia ya alama ya Vidole Mjini Chato Mkoani Geita Desemba 27,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi kitambulisho chake cha Taifa Msajili wa laini za Simu wa kampuni ya simu ya Airtel Michael Martin aliokwenda kusajili Laini ya simu kwa njia ya alama ya Vidole Mjini Chato Mkoani Geita. Desemba 27, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akionyesha simu yake ambayo ametoka kusajili laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole na kisha kuzungumza na Wananchi wa Mjini Chato Mkoani Geita na Watanzania wote ambapo ameongeza muda wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2019 ndio utakuwa mwisho wa zoezi hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Mjini Chato Mkoani Geita na Watanzania wote mara baada ya kusajili laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole ambapo Mhe. Rais ameongeza muda wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2019 ndio utakuwa mwisho wa zoezi hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mjasiriamali wa Chipsi Joseph Wandwi wa Mjini Chato Mkoani Geita mara baada ya kusajili laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole na kuzungumza na Wananchi hao, ambapo Mhe. Rais ameongeza muda wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2019 ndio utakuwa mwisho wa zoezi hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mjasiriamali wa Chipsi Joseph Wandwi wa Mjini Chato Mkoani Geita mara baada ya kusajili laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole na kuzungumza na Wananchi hao, ambapo Mhe. Rais ameongeza muda wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2019 ndio utakuwa mwisho wa zoezi hilo. (PICHA NA IKULU).
No comments:
Post a Comment