By Nazael Mkiramweni, Mwananchi nmkiramweni@mwananchi.co.tz
Dodoma. Kamanda wa Polisi (RPC) Mkoa wa Dodoma nchini Tanzania, Gilles Muroto amesema chanzo cha kifo cha aliyekuwa mmiliki wa Shule za Zamzam mkoani hapa, Sheikh Rashidi Bura ni moyo wake kushindwa kufanya kazi.
Bura (60) aliyekuwa haonekani zaidi ya siku nne alikutwa amekufa juzi Jumatano Desemba 25, 2019 ofisini kwake eneo la Majani ya chai karibu na Nyerere Square jijini Dodoma.
Hata hivyo, wakizungumza na Mwananchi jana Alhamisi Desemba 26, 2019 Ali Rashid Bura (26), mtoto wa marehemu na msemaji wa familia hiyo, Abdillah Mboryo walisema mwili ulikutwa ofisini kwake bila nguo huku ukiwa na makovu matatu mkono wa kushoto, kwenye paja na mgongoni.
Mtoto wa marehemu alisema baada ya kumtafuta maeneo mengine bila mafanikio, alikwenda ofisini kwa baba yake na kukuta mlango ukiwa umefungwa na alipoufungua kwa kuupiga teke ulifunguka. “Ndipo nikauona mwili wa baba ukiwa umeharibika sana huku akiwa amekaa chini na nguo zote zikiwa pembeni,” anasema.
Naye Mboryo alisema: “Mwili wa marehemu ulikuwa na majeraha matatu; mkono wa kushoto, kwenye paja na mgongoni ambayo siwezi kuyazungumzia kwa sababu mimi si polisi lakini niliyaona.”
Leo Ijumaa Desemba 27, 2019 Kamanda Muroto amezungumza na waandishi wa habari kuhusu kifo cha mkurugenzi huyo wa taasisi ya The Dalai Islamic Centre akisema mkurugenzi huyo akiwa ofisini kwake alizidiwa na kufariki dunia baada ya kukosa msaada wa haraka.
Amesema baada ya polisi kufika eneo la tukio na wataalamu wa uchunguzi waligundua hakukuwa na uharibifu wowote katika ofisi yake, walikuta begi dogo lenye nguo chache za safati, simu ikiwa imezima chaji, tiketi ya safari na kwenye waleti kulikuwa na Sh260,000 na vitambulisho vyake.
Muroto amesema taarifa zilizosambaa kwenye mtandao ya kijamii na baadhi ya magazeti kuwa mwili wa marehemu ulikuwa umekatwa baadhi ya viungo na majeraha mbalimbali kwenye mwili wake si za kweli.
Amesema uchunguzi zaidi unafanyika kupitia simu zake ili kubaini kama kuna taarifa za ziada.

No comments:
Post a Comment