ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 17, 2019

SIMBACHAWENE ATEMBELEA OFISI ZA MAKAMU WA RAIS ZA ZANZIBAR

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akipokewa na Mratibu wa shughuli za Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Othman Haji mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Makamu wa Rais zilizopo Tunguu, Zanzibar ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo Pemba
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Tunguu, Zanzibar kabla ya kuelekea Pemba kukagua miradi ya maendeleo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene (katikati) akiongozwa na Afisa Utumishi, Bakari Maulid Bakari (kulia) kutembelea Ofisi za Makamu wa Rais zilizopo Tunguu, Zanzibar ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo Pemba. Kushoto ni Mhasibu kutoka Ofisi hiyo Mohamed Said Mwinyi
Afisa Utumishi Ofisi ya Makamu wa Rais ya Zanzibar Bakari Maulid Bakari (wa pili kushoto) akitoa maelezo kuhusu shughuli za ofisi hiyo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene. Wengine kushoto ni Mhasibu Mohamed said Mwinyi na kulia ni Mratibu Othman Haji. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akiagana na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Tunguu, Zanzibar kabla ya kuelekea Pemba kwa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo.

No comments: