ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 1, 2020

JUMUIYA YA WATANZANIA DMV YAFANIKISHA SHEREHE ZA MKESHA WA MWAKA MPYA


Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV Dj Luka akitoa salamu za mwaka mpya kwenye sherehe za kuaga mwaka 2019 na kukaribisha mwaka mpya 2020 siku ya Jumamosi Dce 31, 2019 katika ukumbi wa The Viking Event Center uliopo Burtonsville, Maryland. Picha zaote na Iska Jojo Studios.

Kutoka kushoto ni makamu wa rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV Bi. Joha Nyang'anyi kulia ni Rais wa Jumuiya hiyo Dj Luka wakimsikiliza mhasibu wa Jumuiya Bi. Lysa Bantu wakati akikabidhi vyeti kwa wadhamini na wadau waliojitokeza kusaidia Jumuiya kwa hali na mali.

Kushoto ni makamu wa Rais Bi Joha Nyang'anyi akittangaza majina ya wanakamati walipochukua tuzo kama shukrani kwa kazi yao ya kusaidia uongozi katika kufanikisha shughuli mbalimbali za Jumuiya. Kati ni Lysa Bantu na kulia ni Dj Luka, Rais wa Jymuiya.

Tuzo zikiendelea.

Katibu msaidizi wa Jumuiya Saria Elvis akifungua sherehe za mkesha wa kuukaribisha mwaka.

Washereheshaji Sunday Shomari (kushoto) kutoka VOA na Maulid Kitenge kutoka Wasafi Media wakinogesha mkesha wa kuukaribisha mwaka mpya wa 2020.

kwa picha zaidi bofya soma zaidi

No comments: