ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 11, 2020

MAKATIBU WAKUU WASTAAFU WA CCM WAHOJIWA

10 Februari, 2020
Dar es Salaam

Makatibu Wakuu Wastaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Yusuf Makamba na Ndg. Abdulrahaman Kinana leo Februari 10, 2020 wamefika katika Ofisi Ndogo za CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam kuitikia wito wa Kamati Ndogo ya Usalama na Maadili inayoongozwa na Ndg. Philip Mangula.

Makatibu Wakuu hao Ndg. Abdulrahman Kinana na Ndg. Yusuf Makamba wamefika katika Ofisi hizo majira ya mchana na kupokelewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Bashiru Ally Kakurwa.


(Pichani) Ndg. Abdulrahman Kinana akiwa ofisini kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndg. Philip Mangula baada ya kuitikia wito wa kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Usalama na Maadili ya CCM.

(Pichani) Ndg. Yusuf Makamba akiagwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndg. Bashiru Ally Kakurwa baada ya kuitikia wito wa Kamati Ndogo ya Usalama na Maadili ya CCM.

Imetolewa na,
HUMPHREY POLEPOLE
KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

No comments: