Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin Mkapa na Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Kikwete, wamewasili jijini Nairobi leo Februari 11, 2020 kushiriki mazishi ya Rais mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya watu wa Kenya, Daniel Toroitich Arap Moi Jumatano Februari 12, 2020.
Mazishi hayo yanatanguliwa na sala maalum ya kuomboleza kifo cha mzee Moi itakayofanyika asubuhi hii kwenye uwanja wa Nayo Kasarani, jijini Nairobi.
Katika uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta, Marais hao wamelakiwa na Balozi wa Tanzaniua nchini Kenya Dkt. Pindi Chana pamoja na maafisa wengine wa serikali ya Kenya.
Marehemu Moi atazikwa Jumatano Februari 12 nyumbani kwake Kabarak, eneo bunge la Rongai, kaunti ya Nakuru. Mzee Moi ambaye aliongoza Kenya kama Rais wa pili kwa kipindi cha miaka 24 alifariki mnamo Febrauri 4, 2020 katika hospitali ya Nairobi ambako alikuwa akipokea matibabu kwa miezi minne.
No comments:
Post a Comment