ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 13, 2020

Rihanna Aogopa Kupanda Helikopta

MSANII wa muziki na mitindo nchini Marekani, Rihanna Fenty, ameweka wazi kuwa, tangu kifo cha nyota wa mpira wa kikapu nchini humo Kobe Bryant, anaogopa kupanda helikopta.

Bryant alipoteza maisha Januari 26 katika ajali ya helikopta akiwa na mtoto wake wa kike Gianna pamoja na watu wengine saba.

Kutokana na tukio hilo lililotikisa dunia, Rihanna amedai hadi sasa amekuwa akiogopa usafiri huo japokuwa awali alikuwa anautumia mara kwa mara.

“Mimi ni msanii pia ni mfanyabiashara, muda mwingi nilikuwa natumia usafiri wa helikopta, lakini tangu Kobe Bryant apate ajali na kupoteza maisha nimekuwa nikiogopa kuutumia usafi huo, namkumbuka sana staa huyo wa kikapu, nitaendelea kuwaombea watoto waliobaki pamoja na mama yao Vanessa,” alisema msanii huyo. GPL

No comments: