Advertisements

Sunday, March 29, 2020

KAMPUNI YA QWIHAYA YATOA ZAIDI YA MILIONI 21 KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO PAWAGA

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa anaongea na waandishi wa habari mara baada ya kupokea msaada kutoka katika Kampuni ya QWIHAYA ya wilaya Mufindi kwa ajili ya wahanga wa mafuriko yaliyotokea katika kitongoji cha Mbingama mkoani Iringa.
Huu ndio msaada wa Mirunda ambayo itaenda kusaidia katika ujenzi wa makazi mapya kwa wananchi wa kitongoji cha Mbingama

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
KAMPUNI ya QWIHAYA GENERAL CO LTD ya mkoani Iringa imetoa msaada wa zaidi ya shilingi milioni 21 kwa wahanga wa mafuliko wa kitongoji cha Mbingama kijiji cha Isele tarafa ya pawaga waliokumbwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea hivi sasa.
Akikabidhi msaada huo Kwa niaba ya mkurugenzi wa kampuni hiyo ,Meneja wa kampuni ya Qwihaya Ntimbwa Mjema alisema kuwa kampuni ya Qwihaya imeguswa na tukio la mafuriko lilowakumba wananchi hao ndio maana wakaamua kutoa msaada huo.
Mjema alisema kuwa wametoa mirunda ya Lori mbili ambayo itasaidia katika ujenzi na unga kwa ajili ya chakula mifuko 30 yenye uzito wa kilo 25 kwa lengo la kusaidia wahanga hao wa mafuriko ambao hawana chakula wala mahala pakulala.
"Tumetoa msaada huo kulinga na taarifa tuliyoipata kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela ili kusaidia wahanga hao pale ambapo kampuni inauwezo kusaidia ndio maana tumetoa mirunda hiyo kwa ajili ya ujenzi pamoja unga kwa ajili ya chakula " alisema Mjema
Mjema alisema kuwa kampuni hiyo imekuwa inatoa misaada Mara kwa Mara kwa wananchi wenye matatizo mbalimbali kwa lengo la kurudisha fadhila kwa wananchi ambao wamekuwa wanunua bidhaa za kampuni hiyo.
Alisema kuwa kampuni Qwihaya imeshasaidia wananchi na taasisi za serikali pamoja na kampuni binafsi kuingiza umeme kwa gharama za kampuni ya Qwihaya.
"Wananchi zaidi ya 7050 tumewasaidia kuingiza umeme kwa gharama za kampuni ya Qwihaya hivyo tumekuwa tunachangia misaada mbalimbali kwa wananchi wenye mahitaji"alisema
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela aliishukuru kampuni ya Qwihaya kwa misaada hiyo ya mirunda na chakula kwa wahanga wa mafuriko wa kitongoji cha mbingama.
Kasesela alisema kuwa wananchi wa waliokumbwa na mafuriko wanahitaji misaada mkubwa ili kuokoa maisha ya awamu ya awali huku wakitafuta njia za kuanza maisha mapya baada ya mafuriko.
"Huuu msaada utasaidia sana kuwasaidia wananchi ambao wamekumbwa na mafuriko wa kitongoji cha Mbingama kwa kuwa bado wanahitaji msaada mkubwa sana hivyo wananchi wengine watakaoguswa wanaweza kuendelea kutuchangia" alisema
Kasesela alisema kuwa tayari serikali imeshatenga eneo maalumu kwa ajili ya kuanzisha kitongoji jipya cha Mbingama mpya na tayari wataalum mbalimbali wa sekta zote wapo katika kitongoji hicho ili kusaidia huduma zote zinapatikana.
Alisema kuwa watendaji ambao wapo katika kitongoji hicho wanaofanya kazi kwa juhudi zote ni wataalamu wa ardhi kwa ajili ya upimaji ardhi na kugawa viwanja kwa wahanga hao, afisa afya kwa ajili ya kusaidia wahanga kupima na kuwatibu afya zao na ulinzi umeimalishwa.
Kasesela alimaliza kwa kushukuru kwa msaada ambao wameupata kutoka kampuni ya Qwihaya iliyopo katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa na kuziomba kampuni nyingine na wadau wengine kuiga mfano wa kampuni ya Qwihaya kwa kusaidia jamii inapokumbwa na majanga mbalimbali.
Alisema kuwa wahanga hao wanahitaji msaada wa mifuko ya saruji,chakula, afya na ujenzi nyumba za muda na baadae kudumu hivyo wadau wanaombwa kuendelea kutuchangia michango mbalimbali.

No comments: